↧
ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU AJULIKANA!
INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013, tuliripoti kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini kuhusu kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia jina la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya huruma kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa Zoom Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa wamepata nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka wamtumie shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU) Baada ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja kati yao akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Mwanzoni alikuwa ana toa hela zake kwa wakala ambaye alisajilia namba hii, lakini baadaye alisafiri na kwenda tarafa nyingine hivyo basi kushindwa kutoa hela kwa sababu namba ameisajili kwa jina ambalo sio lake. Hivyo basi ili kuweza kutoa pesa ilimbidi, ajihamishie salio kutoka katika namba 076390631 kwenda kwenye namba yake halisi ambayo ni 0765283703. Hapo ndipo tulipo weza kumbaini tapeli huyu.
Baada ya kupata taarifa hizi tuliamua kutafuta mbinu za kumkamata kirahisi,ambapo tulimtumia barua pepe, jana jioni kisha ujumbe mfupi wa maneno (SMS) tukimwambia aje Dar Es salaam kuhudhuria semina ya siku tano ya mawakala wa RafikiElimu (Tukamtajia na malipo) Nadhani alistukia kwamba huenda ameshajulikana, akatuma ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka :
↧