Quantcast
Channel: Maisha Times
Viewing all 209 articles
Browse latest View live

Rais Barack Obama leo anaanza rasmi ziara yake ya Afrika!

$
0
0


Rais Barack Obama anaanza ziara yake ya pili rasmi barani Afrika kama rais wa Marekani (26.06.2013). Ataanzia ziara hiyo nchini Senegal, kabla ya kwenda Afrika Kusini na kumalizia Tanzania.
Maratajio yalikuwa makubwa barani humo alipochaguliwa rais huyo mwenye asili ya kiafrika kuwa rais mwaka 2008. Nani kama si yeye ambae angetoa kipaumbele kwa bara la Afrika? Mhula wake wa pili ulipoanza matarajio hayo kidogo yamepwaya.Juhudi zake kuwelekea Afrika zinaonyesha hafifu zikilinganishwa na zile za mtanagulizi wake.
"Nna daamu ya kiafrika mwilini mwangu na historia ya familia yangu mwenyewe inachanganya tangu misiba mpaka mafanikio ya historia ya bara la Afrika." Hayo ndiyo matamshi aliyochagua kuyatamka rais Barack Obama aliefanya ziara fupi nchini Ghana mwaka 2009.
Rais Obama na familia yake walipokaribishwa Ghana 11-07-2009
Furaha na shangwe zilikuwa kubwa alipotaja asili yake ya kiafrika. Kwamba wakati huo huo alilaani rushwa barani Afrika na kushinikiza watu wawajibike, hayo watu waliyafumbia masikio. Nani kama si rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya kiafrika, atakaefungua ukurasa mpya wa sera ya marekani kuelekea Afrika, kuhimiza vitega uchumi vya moja kwa moja na kuinua shughuli za utalii?
Hali lakini imejitokeza vyengine: Migogoro iliyoathiri sekta ya nyumba na uchumi nchini Marekani ilimlazimisha rais Obama anaesalitika zaidi na siasa ya ndani, atangulize mbele masilahi ya kijiografia na kulilenga zaidi bara la Asia na wakati huo huo kuelekeza mawazo yake katika bara la Afrika 

Kauli za wasomi kuhusu ziara hiyo
Professor David Shinn aliyewahi kuwa balozi wa Marekani nchini Ethiopia na Burkina Faso na ambae hivi sasa ni mhadhiri wa siasa za kimataifa katika chuo kikuu cha George Washington anachambua siasa ya Marekani kuelekea Afrika kwa kusema:" Ni kweli kwamba awamu ya kwanza ya utawala wa Obama haikutoa umuhimu mkubwa sana kwa bara la Afrika. Bila ya shaka watu walijiwekea matumaini makubwa.Lakini majukumu muhimu ya siasa ya ndani yalizuka na kufanya iwe shida kushughulikia kwa nguvu masuala ya Afrika.Hilo atalisawazisha katika awamu yake hii ya pili.Ndio maana safari hii ameanza mapema safari hii ndefu".
Hata hivyo si sawa kuwasingizia Obama na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani kwamba hawajishughulishi na masuala ya Afrika. Katika mzozo wa Sudan, Obama aliingiliaa binafsi au aliwatuma wajumbe wake maalum ili kuhakikisha kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan kusini inafanyika kama ilivyopangwa mwaka 2011. Mwaka uliofuatia viongozi wa Afrika walifunga safari hadi Camp David kutokana na mwaliko wa rais Obama, kuhudhuria mkutano wa kundi la mataifa manane tajiri kiviwanda uliopitisha azimio kuhusu mkakati wa kudhamini "usalama wa chakula" duniani.
Mkakati huo unaendelezwa katika nchi 20 zikiwemo Senegal na Tanzania. Hata hatua zinazozusha mabishano zimechukuliwa na serikali ya rais Obama:kwa mfano walipotuma vikosi maalum vya Marekani katika Afrika kati ili kumsaka mkuu wa waasi wa LRA Joseph Kony,au walipoanzisha ujenzi wa vituo vya ndege zinazorzushwa bila ya rubani nchini Athiopia, Niger na Djibuti.
Mwandishi: Ludger Schadomsky/Feleke,Abebe/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Yusuf Saumu-DW

Hii ndio list ya Wabunge Wanaoongoza kwa kuchangia na kutochangia Bungeni!

Waziri Mkuu- Mhe. Mizengo Pinda afute kauli yake- Kituo cha Haki za Binadamu!

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu cha (Legal and Human Right Center) Daktari Helen Kijo-Bisimba (Kulia)
 

KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.

Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.
Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu. Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.

“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga,” alisema Pinda.

Ndugu wanahabari, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimepokea kwa mshituko kauli hii iliyotolewa na kiongozi wa juu serikalini. Maudhui ya kauli hii ni kinyume kabisa cha Katiba ,Sheria za nchi na misingi ya haki za binadamu. katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa yale yanayotokana na vyombo vya dola na jeshi la polisi nchini, ambapo jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu kubwa kupita kiasi katika matukio mbali mbali na kusababisha vifo na kujeruhi watu na hata watu ambao hawakukiuka amri halali ya jeshi hilo.

Matukio haya ya matumizi makubwa ya nguvu za dola ni kinyume na taratibu za utekelezaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 13 (1) Usawa mbele ya sheria , (3)” Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vingine vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria” na (6) (b) ambayo inasema ni “Ni marufuku kwa mtu ………….kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka atakapo thibitika kuwa anayohatia ya kutenda kosa hilo” (e) Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazo mtweza au kumdhalilisha.”

Pia ni Kinyume na kifungu namba 21 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inayounda sura namba 20 ya sheria za Tanzania inayozuia matumizi ya nguvu kupita kiasi na kifungu namba 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma saidizi “Police force and auxiliary Act” Sura namba 322 kama zilivyorekebishwa mwaka 2002, ambayo inaelekeza kukamatwa kwa mtu aliyetenda kosa na si kupigwa. Matumizi makubwa ya nguvu pia ni kinyume na Mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania na inayotambuliwa kwenye Katiba kama Tamko la Haki za Binadamu la Mwaka 1948 na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa Mwaka 1966.

Tungependa kumkumbusha mheshimiwa Waziri Mkuu kuwa Utawala wa sheria unajumuisha serikali, na vyombo vya utekelezaji na ulinzi pamoja na wananchi kuheshimu sheria. Na sio kuvunja sheria kwa vyombo vya usimamizi wa sheria. Tamko hili la Waziri Mkuu limetoa mwanya mkubwa na a nguvu kwa vyombo vya usimamizi wa sheria kuvunja haki za raia. Ikumbwe kuwa yapo matukio mengi ya polisi kutumia vibaya nafasi yao na nguvu waliyonayo katika kuwavunjia haki wananchi kama mauaji yaliyofanywa huko Songea mwezi wa Pili mwaka 2012 ambapo watu wawili waliuwawa na polisi na wengine 48 kujeruhiwa, Iringa mwezi wa tisa 2012 ambapo mtu mmoja aliuwawa (Daudi Mwangosya), Tabora - Usinge 2011 ambapo mtu mmoja aliuwawa. Haya ni baadhi tu ya matokeo ya matumizi makubwa ya nguvu ya polisi. Pamoja na hayo yapo matukio ya polisi kuuwa raia na kuwajeruhi kwenye matukio tofauti tofauti hapa nchini ambayo mpaka sasa Kituo kina matukio ya watu 11 ambao wameuwawa mikononi mwa polisi. Haya yote yanatokea kwa sababu jeshi la polisi limeshindwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na pia kutambua wajibu wao kwa wananchi.

Katika hali hii ya kushtusha, kwenye nchi yenye Amani na Utulivu na kama tunavyopenda kusema kisiwa cha amani, kiongozi huyu wa ngazi za juu anatoa tamko linaloashiria kutoa ruksa kwa Jeshi la polisi kuvunja sheria tena tamko linatolewa hadharani, mbele ya chombo kinachoheshimika kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tofauti na misingi ya Katiba na Haki za Binadamu ni hatari kwa amani na utulivi huo. . Waziri Mkuu anapaswa kuheshimu na kuilinda katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za nchi na kuhakikisha usalama wa raia.

Hivyo basi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Watanzania wanaopenda heshima ya sheria na haki za binadamu na asasi za kiraia tumeendaa waraka unaokusanya saini za watanzania zikimtaka Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda;

1. Kwanza kabisa kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni kubariki polisi kupiga raia katika Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.

2. Kuwaomba radhi Watanzania kwa kile alichosema bungeni.

3. Kulielekeza jeshi la polisi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizoko katika kutekeleza kazi zake za kulinda usalama wa raia na mali zao.

Mpaka sasa tumeshakusanya saini 1000 kudai kauli hii ifutwe ilikulinda maisha ya Watanzania.

Imetolewa kwa Ushirikiano wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu leo Tarehe 26/06/2013.

____________________
Daktari Helen Kijo-Bisimba
Mkurugenzi Mtendaji
 


Kupiga Kura Bofya Link hii http://www.gopetition.com/petitions/wito-kwa-waziri-mkuu-wa-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania/sign.html#se
 

Mfalme Muswati III awasili nchini!

$
0
0
 Mfalme Muswati III wa Swaziland

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo.  Mfalme Mswati wa III ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mfalme Mswati wa III, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati III, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati.

Mfalme wa tatu wa Swatzland amewasili nchini jana na kupokelewa na mwenyeji wake makamu wa rais Dkt Ghalib Bilali aliyeambata na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe. Ujio huo wa Mfalme Muswati ni kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28, 2013.

CCM yadaiwa kuchakachua nakala ya gazeti la Mwananchi kukichafua CHADEMA!

$
0
0
 Nakala iliyochakachuliwa-Gazeti la Mwananchi la Tarehe 25 June 2013. 

 
Nakala halisi ya Gazeti la Mwananchi la Tarehe 25 June 2013. 

Tizama kwa makini kurasa mbili tofauti za nakala ya gazeti la Mwananchi kama zinavyoonekana hapo juu, zote ni nakala za gazeti la Mwananchi la Tarehe 25 June 2013. Wengi kati ya waliofanikiwa kugundua mbinu hiyo chafu ya kuedit nakala hiyo na kuisambaza mitandaoni kwa lengo la kumchafua Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndg. Wilfred Lwakatare na CHADEMA kwa ujumla wameonekana kukihusisha na kukishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusika na uchakachuaji huo kwa lengo la kukipaka matope Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho kimeonekana kuzidi kukubalika zaidi na wananchi kila kukicha hata kuinyima usingizi kabisa Serikali ya CCM http://www.facebook.com/chadema.saut/posts/379868878780837?comment_id=1912230&offset=0&total_comments=11&notif_t=feed_comment_reply
 

Wabongo na Mandela: Tatizo ni nini?

$
0
0
Katika kipindi chote hiki cha kuumwa kwa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kumekuwa kukizushwa habari za kifo chake mara nyingi zaidi kuliko hata habari za hali ya kuumwa sambamba na maendeleo ya hali yake.  Baadhi ya waandishi na hasa Bloggers wameendelea kudakia habari za uongo na kutangaza kuwa kiongozi huyu amefariki bila kuwa na uhakika na hivyo kuwafanya wasomaji washindwe kujua nini hasa kinaendelea.

Maisha Times inawaomba waandishi na bloggers wengine kuwa na subira na kujaribu kufuatilia vyombo vya kuaminika kwenye ishu muhimu kama hii. Si jambo la busara kuendelea kutoa habari za uongo ili mradi tu watu wasome ulichoandika. Tubadilike!

Leo hii, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameuambia umma kuwa hali ya Mandela imeimarika kwa kiasi. Rais Zuma pia amesitisha safari yake ya Msumbiji ili akaonane na Mandela na madaktari wake.

Maisha Times itaendelea kukupa habari za uhakika kuhusiana na hali ya kiongozi huyu wa Afrika na muasisi wa demokrasia ya Afrika Kusini.

Chuo Kikuu Huria kumtunukia Rais Obama shahada ya heshima ya Uzamivu (PHD)

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kukuu Huria Prof. Tolly Mbwete

Kufuatia ujio wa Rais wa Marekani Barrack Obama nchini Tanzania Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimeamua kumtunukia Rais huyo Shahada ya heshima Uzamivu (PHD). 
Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete ambaye aliongeza na kusema kwamba tayari Mkuu wa Chuo hicho Dr. Asha Rose Migiro ameshapewa taarifa hiyo na kuikubali kwahiyo kinachofuata ni kusubiri ujio wa rais Barack Obama ili waweze kumtunukia Shahada hiyo ya Heshima kutokana na juhudi zake za kupigania maendeleo ya jamii.


Sasa Barabara ya "Ocean Road" kuitwa "Barack Obama Road"!

$
0
0
Barabara ya Ocean Road ambayo itabadilishwa jina na kuitwa Barack Obama Road

Kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadick Meck Sadick

Hayo yamesemwa na na Kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadick Meck Sadick ambaye aliongeza na kusema kwamba uamuzi wa kubadili jina la barabara hiyo utafanyika ikiwa ni zawadi ya wakazi wa ilala kwa rais Barack Obama.


Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda kesi na kuthibitisha kwamba Waziri Mkuu ni "Mpumbavu"

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu)
Taarifa zilizoifikia Maisha Times muda sio mrefu zinaripoti kwamba asubuhi ya leo Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye
alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.

Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.


Angalia Video: Wakenya wakereka na kitendo cha Obama kutokwenda Kenya!

Bonus Photo: Ni Furaha iliyoje kuonana na Obama!

$
0
0
Pichani ni mmoja ya wapenzi wa rais Barack Obama wa marekani akionyesha Furaha yake na kumkumbatia kwa namna ya pekee pindi alipobahatika kukutana nae uso kwa uso. 

Sipati picha iwapo kama ikitokea mtu akaonyesha furaha yake na kumlaki rais Obama kwa namna hiyo nchini Tanzania itakuwaje!


Rais Barack Obama awasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere

Why are we pretending??!! Obama Should be told the Truth about Tanzania!!

$
0
0
The other side of Tanzania!


In most areas, this is the real life for the majority of Tanzanians.






























It's Obama time, time to clean our city!

This is our Democracy! 




Our Country is Beautiful but........
























Obama ameondoka: Sasa Kuchafua jiji, Uzururaji, Ombaomba, Foleni zisizo za lazima nk nk. Ruksa!

Basi la Saibaba lapata ajali wakati likitokea Moshi kuja Dar!

$
0
0

Basi lifanyalo Safari zake kati ya Mkoa wa Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam lijulikanalo kama "Sai Baba" leo limepata ajali wakati likiwa njiani kuelekea jijini Dar es salaam. Maisha Times itazidi kuwapa habari zaidi juu ya waliojeruhiwa/kufa katika ajali hiyo.

Kumekucha: Mbinu chafu za CCM kuvuruga uchaguzi mdogo wa Madiwani Arusha zafichuka!!!!

$
0
0

Naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba Kushoto na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye.

Habari za kuaminika zinasema kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameingiza nchini makontena ya Nguo-Gwanda, T-Shirts, Kofia, Kadi, Bendera za CHADEMA nk kutoka nchini China.
Mavazi sambamba na kadi hizo yatavaliwa na kutumika maalum kufanya fujo na matukio ya uvunjifu wa amani katika sehemu mbalimbali nchini haswa haswa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha mnamo tarehe 14/7/2013 ili kusingizia na kutengeneza mazingira kwamba vurugu hizo zimefanywa na Viongozi, Wanachama na Washabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Hizo ni baadhi ya mbinu chafu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uratibu wa Naibu katibu mkuu wa chama hicho Mwigulu Nchemba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ili kuvuruga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mnamo tarehe 14/7/2013, mbinu ambazo tayari Viongozi wa CHADEMA wamepewa taarifa na uthibitisho kutoka kwa wasamaria wema waliomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watakutana mapema ili kujadiliana na kutoa tamko maalum kwa vyombo vya habari na umma juu ya suala hilo.


Chanzo Jf http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/480637-mbinu-chafu-za-ccm-kuvuruga-uchaguzi-mdogo-wa-madiwani-arusha-zafichuka.html

Ziara ya Rais Barack Obama yathibitisha wazi tatizo la ajira nchini Tanzania!

$
0
0








Pichani: Umati mkubwa wa Wananchi waliojitokeza kwa wingi kukumlaki, kumpokea na kumuaga Rais Barack Obama wa marekani katika siku na muda ambao wananchi walitakiwa kuwa katika sehemu zao za kazi au shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa unaweza kutumika kuthibitisha tatizo la ukosefu wa ajira nchini Tanzania!



Wamisri wacharuka Wamshinikiza Rais Mohamed Morsy kung'atuka!

$
0
0








Rais wa Misri Mohammed Mosri anaendelea kukabiliwa na shinikizo kali huku maafisa zaidi wa serikali yake wakiendelea kujiuzulu nao waandamanaji wakianza kukusanyika tena katika bustani ya Tahrir.
Msemaji wa rais na mwenzake wa baraza la mawaziri nao pia wamejiuzulu , baada ya mawaziri sita kuondoka serikali mwishoni mwa wiki kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali.

Awali taarifa ya rais ilipinga vikali onyo la jeshi dhidi ya utawala wa Morsi kwa kumpa masaa 48 kusuluhisha mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo.
Chama rasmi cha upinzani National Salvation Front, kimesema kinaunga mkono tamko la jeshi lakini katu hakiungi mkono mapinduzi ya kijeshi.
Taarifa hiyo ya rais imesema kuwa hatua hiyo ya jeshi kuingilia kati itazua hali ya suitofahamu zaidi.
Jeshi limekanusha madai kuwa makataa hayo ni sawa mapinduzi ya kijeshi.
Serikali imesema kuwa Morsi amewasiliana na rais Barack Obama kuhusu hali ya kisiasa inayoshuhudiwa Misri.
Wakati huohuo, shirika la habari la kitaifa Misri, limeripoti kuwa waziri wa mambo ya nje Mohamed Kamel Amr amejiuzulu.
Ikiwa ombi lake litakubaliwa, atakuwa mmoja wa mawaziri wengine watano ambao wamejiuzulu kufuatia mgogoro huo wa kisiasa.
Mnamo jumapili, mamilioni walifanya maandamano wakimtaka rais ajiuzulu.
Maandamano mengine makubwa yalishuhudiwa Jumatatu na kuendelea mpaka siku ya leo (Alhamisi) huku ripoti zikisema kuwa watu wanane waliuawa wakati waandamanaji walipovamia makao makuu ya chama tawala cha Muslim Brotherhood.
Wapinzani wa Morsi, wanamkosoa kwa kuweka maslahi ya chama mbele huku akiwapuuza wale wasiounga chama hicho.
Morsi alichaguliwa kama rais wa kwanza wa kiisilamu katika uchaguzi wa mwezi Juni mwaka 2012 tarehe 30 baada ya kushinda uchaguzi uliotazamiwa na wengi kuwa huru na wa haki baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak.

Manzese hapakaliki: Ni vita kati ya Wamachinga na Polisi, Ofisi ya CCM yachomwa moto!

$
0
0


Habari zilizoifikia maisha Times Blog dakika chache zilizopita zinaripoti kwamba hali si shwari katika eneo la Manzese jijini Dar es salaam, Polisi wanapambana na wafanyabiashara wadogo wadogo (Wamachinga) waliovamia na kufanya biashara eneo la barabara ya Morogoro Road katika eneo hilo kinyume na amri ya Jeshi la Polisi ya kupiga marufuku wafanyabiashara hao kufanya biashara katika eneo hilo.

Kuna habari ambayo haijathibitishwa inayosema kwamba Vurugu hizo zimepelekea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo kuchomwa moto.

Endelea kufuatilia Maisha Times Blog na punde tutakujuza zaidi kuhusiana na kile kinachoendelea.

Kunani misaada ya Lowassa Misikitini na Makanisani??!!

$
0
0
















Watu wengi wamekuwa wakijiuliza na wengine kuhoji aliyekuwa waziri mkuu Mhe. Edward Lowassa ana biashara gani haswa?! Kwani ni kwa muda mrefu sasa amekuwa akipita huku na huko katika kona zote za Tanzania kutoa misaada kuanzia Misikitini, Makanisani, Vikundi vya dini mbalimbali nk nk na binafsi naliona kuwa hilo ni jambo jema sana kwani "kutoa ni moyo na si utajiri" lakini swali la kuntu linakuja ni je fedha zote hizo zinatoka katika mfuko gani haswa?
Viewing all 209 articles
Browse latest View live