↧
Bonus Photo: Kilimo Kwanza, Je tutafika?!
↧
Tweet ya CCM yenye Kingereza Kibovu iliyogeuka Kichekesho Kenya!
Chini ni Baadhi ya Comments zilizoandikwa na wadau baada ya Tweet hiyo:
>This is very disappointing and the reason why there are many Division 0's!!
>Mhhh so sad, its rather unfortunate aki, they should be banned from writing English comments, this is a serious offence to the language..lol
>No way could this be his Nyumba Ndogo coz seriously this is not serious at all. A disgrace once again to Tanzania.
> Did ccm really tweet this?!.. no wonder they are not serious...
Imetoka: https://twitter.com/ccm_tanzania/status/309229895114956800
↧
↧
Skendo ya Mtanzania anayetuhumiwa kukamatwa S.A na Madawa ya Kulevya ukweli ni huu!
Baada ya habari za kukamatwa kwa mwadada Mtanzania Agness Gerald na Melisa Edward kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 kuenea na kuthibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Godfrey Nzowa Agness Gerald ambaye wengi wamedai kwamba ni Aggy Masogange ambae yuko nchini South Africa mpaka dakika hii (haijajulikana kama ni yeye kweli) ameonekana akiendelea kuandika kupitia mtandao wa instagram licha ya kutangazwa kwa habari hizo za kukamatwa kwake.
Masaa machache yaliyopita Aggy amepost picha (hiyo hapo juu) na comments zake ndio kama zinavyoonekana hapo juu!
Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni je, Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya Uongo kuhusu Mtanzania huyo aliyekamatwa na Madawa ya Kulevya nchini Africa Kusini?!
↧
TAHADHARI: Mafuta ya Ubuyu hayafai kwa matumizi ya binadamu, yanasababisha Saratani!
Mbegu za Ubuyu
Baada ya kuonya wananchi wanaotumia dawa za tiba mbadala ambazo hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), sasa inawataka wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa kama dawa.
Akizungumza siku chache zilizopita katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana tindikali ya mafuta.
Alifafanua katika maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini kupata saratani za aina tofauti tofauti.
"Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wajasiriamali wanaouza mafuta ya ubuyu kama dawa, kwa kuwaelekeza wananchi kunywa. Napenda kuwataarifu kuwa mafuta hayo ni hatari kwani yana tindikali ya mafuta," alisema.
Mwandishi alipata sampuli ya vielelezo vya matumizi yake na manufaa yake mwilini, kama inayotangazwa na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali na hata katika mitandao.
"Ni mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu (au kokwa). Hukamuliwa kiini chake na kutoa mafuta. Yana ubora kuliko mafuta mengine ya kupikia, yana Vitamin A, B, C, D na F. Pia yanatibu magonjwa mbalimbali," kielelezo kimoja kilinadi ubora wake katika mitandao ya jamii.
Mafuta hayo yamedaiwa kutengeneza seli zote ndani ya mwili, kuzuia ngozi isiharibike wala kupata

makunyanzi, kuondoa mafuta ndani ya mishipa ya damu na yanapunguza uzito uliozidi.
Pia inadaiwa yanarutubisha ini na figo, yanaleta hamu ya kula, yanaimarisha mifupa, kucha na nywele, yanaongeza kinga ya mwili (CD4), yanaondoa sumu na yanatengeneza sukari iwe katika kiwango kinachotakiwa.
Maelezo hayo yameendelea kusifu kwamba yanasaidia kuona vizuri na kujenga kumbukumbu, yanapunguza vitambi na matumbo makubwa, yana virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini.
Katika ngozi yametajwa kuondoa madoa, chunusi, fangasi, upele, mba na muwasho, yanafaa kwa walemavu wa ngozi (albino). Pia huondoa hamu ya kutumia dawa za kulevya na kuponyesha vidonda vya tumbo.
"Endelea kutumia mafuta bora ya ubuyu, ni bidhaa asilia ya kitanzania. Ni mafuta yasiyochanganywa na kitu chochote, ni mafuta asilia," yamesifiwa katika maelezo hayo.
Mtumiaji ameelezwa kama ana ugonjwa wa kisukari, atumie kijiko cha chakula kimoja tu. Anatakiwa kutumia dozi hiyo ya kwanza nusu saa kabla ya kula chochote kwa muda wa siku 15.
Dozi ya pili na ya tatu kwa wagonjwa hao, inatakiwa kufuata baada ya siku 15 kisha mgonjwa apumzike wiki moja, huku akiendelea kupima kila wiki. Kipimo hapo ni cha hospitali.
Kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, figo na ini, wameelekezwa na wajasiriamali hao kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja kabla hajala chochote kwa muda wa siku 15 kwa dozi ya kwanza.
Baada ya hapo, mgonjwa anapumzika wiki moja kisha siku 15 zinazofuata dozi ya pili, mapumziko wiki moja halafu siku 15 nyingine dozi ya tatu.
Maelezo ya dozi hiyo ya kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, yanaendelea kumtaka mgonjwa baada ya dozi ya tatu, aanze kunywa kila wiki mara moja kijiko cha chakula kimoja asubuhi, tena nusu saa kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne.
Dozi inaendelea ambapo mgonjwa atatakiwa kunywa kijiko kimoja cha chakula kila mwezi mara moja asubuhi, kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne, kisha kunywa kila mwezi mara moja, asubihi kabla hajala chochote kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Kwa utoaji wa sumu, mgonjwa ametakiwa kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kila siku kwa muda wa siku 14, kisha kunywa kila mwezi mara moja kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Kwa kuongeza CD4 mwilini, ametakiwa kupata kijiko cha chakula kimoja asubuhi nusu saa kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja nusu saa kabla ya kula chakula cha usiku kwa muda wa miezi mitatu.
"Mgonjwa aanze kunywa baada ya kipimo cha mwisho (cha CD4) alichopima. Mafuta yanapatikana kuanzia ujazo wa lita moja na zaidi," imesifiwa dawa hiyo.
TFDA imeonya kuibuka kwa tabia ya wananchi kutaka matibabu ya haraka, kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutaka utajiri wa haraka, na imehadharisha ni vema kabla ya kutumia dawa zinazoibuka kila siku, waulize kama zina ubora kwa afya zao.
"Nawasihi wananchi kuacha kukimbilia dawa ngeni mara tu baada ya kutangazwa kama haya Mafuta ya Ubuyu, yamekuwa yakielezwa ni dawa na wajasiriamali tu, na wengi wamekuwa wakitumia bila kusikiliza mamlaka husika zinasemaje," alisisitiza.
Semwanza alisema Mamlaka hiyo iko katika mkakati wa kuanza kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya mafuta hayo, ambayo wengi wanayaamini na kuyanywa kama dawa.
Kwa mujibu wa Semwanza, baada ya kupima mafuta hayo na kubaini hatari hiyo, waligundua pia inawezekana tindikali hiyo kutenganishwa na mafuta hayo, lakini imebainika utaalamu na teknolojia hiyo haipo nchini.
Hata hivyo, alisema Mamlaka hiyo haijabaini madhara ya matumizi mengine ya mafuta hayo kama kipodozi.
Kutokana na mvuto huo wa kibiashara, na shauku ya kupona haraka ya wananchi, Semwanza alisema TFDA imekuwa ikifanya msako wa dawa mbalimbali zinaouzwa na wajasiriamali katika maonesho hayo.
Alisema kuwa kuna baadhi ya waandaaji wanaowaalika wajasiriamali bila kufuata kanuni na sheria za kuingiza dawa hizo katika maonesho.
Kwa mujibu wa Semwanza, wanakagua dawa na kama wakikuta hazijathibitishwa na TFDA na mamlaka nyingine, wanamuamuru mjasiriamali kuacha kuzitangaza mpaka apate kibali na kuwaasa wanaowaleta wajasiriamali katika maonesho hayo ya kimataifa kuhakikisha wanafuata vigezo.
Wiki iliyopita TFDA, ilionya wananchi dhidi ya matumizi ya dawa za tiba mbadala, zikiwamo zinazokuza maumbile, ambazo bado hazijasajiliwa na Mamlaka hiyo baada ya kuchunguza usalama, ubora na ufanisi wa dawa hizo.
Mamlaka hiyo ilieleza kuwa, ilitoa nafasi ya watoa tiba mbadala kwenda kusajili dawa zao, lakini mwitiko umekuwa hafifu.
TDFA yenye dhamana ya kusimamia ubora na usalama wa bidhaa za vyakula na dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za mitishamba, vipodozi na vifaa tiba vinavyouzwa katika soko la Tanzania, imeeleza kuwa watoa huduma wa tiba mbadala, wengi hawako tayari kubainisha aina ya mchanganyiko wa dawa hizo jambo ambalo ni hatari kwa walaji.

Kujua mengi ya zaidi bofya http://www.tfda.or.tz/au wasiliana na mamlaka ya Chakula na Dawa kupitia simu zifuatazo 0658 445222, 0685 701735 na 0777 700002.
↧
Mama mzazi wa Msanii Frof. Jay amefariki dunia usiku wa kuamkia leo!
Pichani Msanii Prof. Jay akiwa na marehemu mama yake Bi Rosemary Majanjara.
Habari zilizoifikia Maisha Times Blog zinaripoti kwamba mama mzazi wa Msanii nguli wa Muziki wa Bongo Flavour (Hip Hop) Frof. Jay amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Tumbi muda mfupi baada ya kupata Ajali ya gari maeneo ya Mbezi mwisho wakati akitokea akitokea nyumbani.
Maisha Times inatoa pole kwa Msanii Prof. Jay na wanafamilia wote. Mungu ailaze roho ya mpendwa mama yetu mahali mema peponi Amen.
↧
↧
Tendwa Kukifuta CHADEMA!
Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa
Hatimaye msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria, katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.
Msajili huyo amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.
Source: JF
↧
NCCR Mageuzi yakataa kuungana na CHADEMA kuunda Halmashauri!
Makubaliano baina ya CHADEMA na NCCR ya kushirikiana kuunda halmashauri ya wilaya ya uvinza yameingia dosari baada ya uongozi wa juu wa NCCR kukataa kushirikiana na CHADEMA yenye viti 7, NCCR viti 5 na CCM viti 5.
Habari zaidi zinaripoti kwamba Uongozi wa Juu wa CHAMA Cha NCCR-Mageuzi umepinga makubaliano ya kuongoza kwa pamoja Halmashauri ya Wilaya Uvinza Kati ya CHADEMA na chama hicho. Makubaliano ya awali ilikuwa ni kwa CHADEMA kurejesha fomu za uenyekiti, NCCR-Mageuzi umakamu. CHADEMA imerejesha, NCCR-Mageuzi imerejesha ya uenyekiti pia. Hivyo nafasi ya makamu Mwenyekiti imebaki na mgombea wa CCM tu.
Makubaliano yalikuwa CHADEMA watoe mwenyekiti na NCCR watoe makamu, lakini cha kusikitisha, CHADEMA na NCCR wamerudisha wote fomu za uenyekiti huku CCM pekee akirudisha fomu ya makamu mwenyekiti.
↧
Udhoofu wa CCM wadhihirika ziara ya Rais Kikwete - Kagera
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida, Mamlaka za Serikali mjini Bukoba, baada ya kuona upepo wa kisiasa mjini Bukoba kwamba kuna hatari kubwa Rais Kikwete akakosa wananchi wa kumpokea na kushiriki naye kwenye shughuli za uzinduzi wa Mahakama na jengo la KCU, Wakuu wa shule za Sekondari zote mjini Bukoba waliamrishwa kufunga shughuli za masomo kuanzia muda wa saa6 mchana siku ya tarehe 24/7/2013, na kuamru wanafunzi warudi nyumbani, wavae nguo za kiraia ili wafike Uwanja wa ndege na maeneo yote ambapo Rais atakapokuwa.
Kwa sababu hiyo, JK alipokewa na idadi kubwa ya wanafunzi, chini ya miaka 18, huku wakiwa katika mavazi ya kiraia na kuwaweka katika hatari ya ulinzi na usalama wao.
Wazazi wamelalamikia suala hili na tunajipanga kupeleka malalamishi rasmi kwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Bukoba kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa kukubali kuingiliwa na mambo ya kisiasa.
Chanzo JF
↧
Waraka mzito kutoka kwa Msanii Kala Jeremiah kumhusu Edward Lowassa ambao umewashtua Wengi!
TANGAZO KWA UMMA
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND. KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI. KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. Walipiga dili waka msakizia Lowasa ili kuficha siri kali. NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika. HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.
Tafakari chukua hatua
Chanzo: http://www.sammisago.com/2013/07/mustread-waraka-mzito-kutoka-kwa-kala.html?spref=tw&m=1
↧
↧
Wafungwa wa Madawa ya Kulevya Wafunguka
Katika barua ifuatayo, mfungwa mmojawapo anaeshikiliwa huko Hong Kong, ametoa maelezo juu ya biashara hiyo na baadhi ya wahusika wake. Ameelezea pia jinsi alivyojiingiza kwenye biashara hiyo haramu, kukamatwa kwake, na vita aliyoianza dhidi ya biashara hiyo.
Barua kwa lugha ya kiswahili
Barua kwa lugha ya kiingereza
↧
Sakata la Madawa ya Kulevya nchini- Mawaziri na Vigogo wa CCM watajwa kuhusika!
Siku chache baada ya kijana mmoja wa Kitanzania aliyeko gerezani mjini Hong kong nchini China kuandika waraka akielezea sababu za yeye kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya na kuwataja baadhi ya vigogo wa dawa hizo nchini, hali imeendelea kuwa tete baada ya mawaziri wawili kuhusishwa katika biashara hiyo.
Mbali na mawaziri hao wawili (majina tunayo) pia wabunge watatu wa viti maalumu wakiwemo wachungaji wakubwa hapa nchini (majina yanahifadhiwa) nao wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo huku wakitumia vitambulisho vya Ikulu ili kufanikisha kazi zao.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki katika mhadhara wa kongamano la kidini kwenye Ukumbi wa Kanisa la TAG Uyole jijini Mbeya na wanafunzi wawili ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo (majina tunayo) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na St. Gasper cha Morogoro wakati wakisalimisha kilo tano za heroine.
Dawa ambazo walikuwa wakizisambaza jijini Mbeya ambapo baada ya kuguswa na neno la Mungu waliamua kuzisalimisha mbele ya kanisa hilo.
Wakizungumza katika kongamano hilo vijana hao walisema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakitumiwa kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikiwanufaisha vigogo wa dawa za kulevya ilhali wao wakiishia magerezani.
Sababu za kusalimisha
“Tumeamua kujisalimisha mbele ya Mungu, tumeamua kuzisalimisha dawa hizi mbele ya Mungu, tunatubu kwa dhambi tulizozifanya, tumeiangamiza jamii isiyo na hatia...tunatubu mbele ya Mungu,” alisema mmoja wa vijana hao (jina tunalo) huku akibubujikwa na machozi mbele ya umati wa waumini waliohudhuria kongamano hilo.
Akitoa ushuhuda mbele ya ya waumini waliokuwa katika kongamano hilo ambalo liliongozwa na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga na Mchungaji Daud Mwalonde wa Kanisa la TAG Calvary Tempo, mmoja wa vijana hao alisema kuwa amekuwa katika biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ambapo amesafiri katika nchi mbalimbali za Asia kama vile Afghanistan, India na nchi kadhaa za Bara la Afrika.
Alisema kuwa, huko walichukua na kuzisafirisha dawa hizo na kupata ujira mdogo ambao haukuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku hivyo wameamua kujisalimisha kwa kuwa wanaamini kuwa maisha ya hapa duniani wameshindwa kufanikiwa na mbele ya Mungu wataingia motoni.
Alisema kuwa, yeye pamoja na mwenzake walikuwa wamesimama Uyole wakitokea jijini Dar es Salaam kwa mtu mmoja waliyemtambulisha (jina linahifadhiwa) ambako ndiko hufanya kituo kabla ya kusambaza mzigo huo katika vituo vya mipaka ya Tunduma hasa Wilaya ya Momba na Kasumulu Kyela ambako mzigo husafirisha nje ya nchi.
Mawaziri wamo
Alibainisha kuwa, katika biashara hiyo wamo mawaziri wawili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano nchini akiwemo mmoja anayehusishwa na ugombea urais mwaka 2015 na Naibu Waziri katika moja ya Wizara za serikali ya Jamhuri ya Muungano (majina tunayo). Aidha, kijana huyo alisema kuwa mtandao huu wa dawa za kulevya pia unawahusisha baadhi ya wachungaji maarufu nchini (majina tunayo) ambao alidai wanapokuwa katika biashara hiyo hutumia vitambulisho vya Ikulu na kufanikiwa kupenya maeneo mbalimbali nyeti ili kufanikiwa kupitisha dawa za kulevya.Akiendelea kutoa, ushuhuda katika kongamano hilo ambalo lililenga kuombea amani na utulivu wa nchi, alisema kuwa baadhi ya klabu za kusaidia watoto wagonjwa wanaosafirishwa kwa ajili ya matibabu nje ya nchi pia zinahusishwa katika usafirishaji wa dawa za kulevya.
Aliwataja baadhi ya wabunge watatu wa viti maalumu na wabunge wastaafu kutoka chama tawala (majina yanahifadhiwa) ambao humiliki maduka makubwa katika majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Tanga, Arusha, Dodoma, Mwanza na baadhi ya nchi za Kiarabu ambapo walidaiwa huwa wanawatumia baadhi ya wasanii na waimbaji wa nyimbo za Bongo fleva zikiwemo za Injili katika usambazaji wa dawa hizo kwa mashabiki.Mara baada ya kusalimisha dawa hizo aina ya heroine, Mchungaji Mwamalanga aliamuru dawa hizo zichomwe moto na kutumbukizwa katika shimo la choo ambapo vijana hao baadaye viongozi wa dini waliwahifadhi.
Akizungumza sababu za kuzichoma moto na kuzitunbukiza katika shimo la choo badala ya kuzisalimisha kwa Tume Inayohusika na Uratibu wa Dawa za Kulevya nchini ili kuzihakiki, Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa waliamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa dawa hizo zimekuwa zikirejea mikononi mwa watumiaji baada ya kukamatwa.Alisema kuwa, kulingana na taarifa walizonazo ni kwamba mara kadhaa watuhumiwa wa dawa za kulevya hukamatwa lakini dawa hizo zimekuwa zikirudi kwa watumiaji na kufanya jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya kugonga mwamba.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Rage alisema Mbunge yeyote hawezi kushtakiwa mahakamani anapotekeleza wajibu wake ndani ya Bunge hivyo kituo hicho kinapaswa kuwaacha wabunge na viongozi wa Serikali wafanye kazi zao bila vitisho.
Alisema, kabla kituo hicho hakijafikia uamuzi huo, kinapaswa kupitia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge namba tatu pamoja na Katiba ya nchi Ibara ya 100 ili kujiridhisha kama kuna uhalali wa kumfungulia mashtaka Bw. Pinda.
“Kama LHRC wamekerwa na matamshi ya Waziri Mkuu aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Serikali, waende kulalamika kwa Spika wa Bunge si kumfungilia mashtaka kwa kigezo cha kuangalia haki.
“Tusiangalie haki peke yake bila wajibu, suala hili linakuzwa kwa shinikizo la kisiasa jambo ambalo halipaswi kushabikiwa hata kidogo, mtu yeyote ambaye atakataa kutii amri halali, polisi anaruhusiwa kutumia nguvu ya ziada,” alisema.
Bw. Rage alikwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, yupo tayari kumsaidia Bw. Pinda akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao wanamuunga mkono kwa kuhakikisha kama Waziri Mkuu atafikishwa mahakamani, watasimamisha wanasheria makini wa kumtetea na kushinda.
“Kama leo hii tutaruhusu LHRC imfungulie mashtaka Waziri Mkuu bila sababu za msingi mbali ya kulinda sheria za nchi, upo uwezekano mkubwa wa wabunge wengine kufanyiwa kitendo kama hicho...mbunge anapozungumza ndani ya Bunge haruhusiwi kushtakiwa kwa kauli yake,” alisema Bw. Rage.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi nchini lina kaulimbiu inayosema ‘Utii wa Sheria bila Shuruti’, hivyo watu wote wanaokataa kutii amri halali wanatambua madhara yanayoweza kutokana na ukiukwaji huo hivyo alichosema Bw. Pinda ni sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa Uboreshaji na Utetezi kutoka LHRC, Bw. Harold Sungusia, alisema wanakamilisha taratibu za kufungua mashtaka dhidi ya Bw. Pinda katika Makahama Kuu.
Alisema Bw. Pinda amevunja katiba ya nchi kwa kusema kuwa, “Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua kukahidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee wote tukubaliane kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria sasa kama wewe ukijifanya jeuri utapigwa tu.
“Na miminasema muwapige tu kwasababu hakuna namna nyingine maana tumechoka”, alisema Bw. Pinda ambapo Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kauli hiyo ni kinyume na Katiba, Sheria za nchi na misingi ya Haki za Binadamu.

Bw. Sungusia aliongeza kuwa, kituo hicho kilitegemea Bw. Pinda angefuta kauli yake ambayo aliitoa katika Bunge la Bajeti lililoisha hivi karibuni lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
↧
Breaking News: CCM yafukuza madiwani Kagera!
Wakati mgogoro kati ya Meya wa Bukoba na Balozi Kagasheki ambaye pia ni waziri wa maliasili na utalii ukiendelea kufuka moshi hali imeendelea kuwa tete kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kagera baada ya Chama hicho kulazimika kuwafukuza na kuwavua Uongozi madiwani8, hatua hiyo imetokana na kile kinachosemwa na chama hicho kwamba ni kitendo cha madiwani hao kukivuruga chama hicho na kukaidi kauli ya rais iliyokuwa ikilenga katika kumaliza mgogoro kati ya Meya wa Bukoba na Balozi Kagasheki.
↧
Maandamano ya CHADEMA kumng'oa Meya wa Ilemela yafanyika jijini Mwanza!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, kimeitisha na kufanya maandamano makubwa ya amani leo kwa ajili ya kushinikiza kung’olewa kwa meya wa manispaa hiyo Henry Matata anayedaiwa kuchaguliwa kinyume cha sheria. Tangu mida ya saa4 asubuhi kumeonekana umati mkubwa wa wa watu wakiwa barabarani wakitokea eneo la Buzuruga kuelekea katika viwanja vya Furahisha ambapo maandamano hayo yatapokelewa na mkuu wa mkoa.
Awali akitangaza maandamano hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Mwanza, Ofisa Operesheni wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema yataungwa mkono na maelfu ya wananchi wa Nyamagana.Taarifa za awali kuhusiana na maandamano hayo wali lisema maandamano hayo yataanzia Buzuruga saa 4:00 asubuhi kisha kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, katika uwanja wa Furahisha, na kwamba unahitajika kufanyika upya uchaguzi wa meya na naibu wake.
Tungaraza aliyeongozana na ofisa wa chama kanda hiyo, Meshack Mikael, pamoja na katibu wa mbunge wa Ilemela, Laban Agrey, alisema maandamano hayo yanahusisha pia kupinga kufukuzwa kinyemela madiwani watatu wa chama hicho.
Madiwani waliofukuzwa na meya wa manispaa hiyo kinyume cha sheria ni Abubakar Kapera (Nyamanoro), Malietha Chenyenge (Ilemela) na Dany Kahungu wa kata ya Kirumba.
“CHADEMA tumeitisha maandamano makubwa hapo kwa lengo la kumkataa meya wa Ilemela na kushinikiza uchaguzi ufanyike upya.
“Matata amechaguliwa bila kukidhi akidi ya madiwani wa manispaa hiyo ambayo ni theluthi mbili ya madiwani wote 14, hivyo siyo meya.
“Lakini maandamano haya yatalenga pia kupinga Matata kuwafukuza madiwani wetu kinyemela. Sheria zinasema diwani atakosa sifa baada ya kutohudhuria mfululizo vikao vitatu vya Baraza la Madiwani, lakini Matata aliyechaguliwa kinyume cha sheria aliwafukuza ndani ya wiki moja baada ya kuchaguliwa,” alisema.
Alisema CHADEMA pamoja na wananchi wa Ilemela wanahitaji kufanyika upya kwa uchaguzi wa meya na naibu wake na kwamba kama kweli madiwani hao wamefukuzwa kihalali wapewe barua za kufukuzwa kwao na tume ya uchaguzi itangaze kata hizo kuwa wazi.
“Kuna taarifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alishaandika barua ya kutengua uamuzi wa kufukuzwa madiwani hao na barua hiyo ‘imekaliwa’ na mkuu wa mkoa,”alisema.
Naye katibu wa Highness Kiwia, Laban Aggrey, kwa niaba ya mbunge huyo alisema kuwa maandamano hayo yataanzia Buzuruga kisha kupita barabara ya Nyerere, Mlango mmoja, Uhuru, Nkrumah, Balewa na kuishia uwanja wa Furahisha.
“Polisi wameshabariki kufanyika maandamano yetu, hivyo ofisi ya mbunge wa Ilemela inawasihi sana wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kudai haki yao iliyoporwa kinyume cha sheria,” alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, alisema maandamano hayo ya CHADEMA yameruhusiwa na jeshi lake.
“Haya maandamano tumeyaruhusu kabisa yafanyike, maana kama watu wanasema wanadai haki yao kwa nini tuwazuie? Tumewapangia maeneo ya kupita maandamano haya hadi huko Furahisha,” alisema Mangu.
Uchaguzi wa meya wa Ilemela uliofanyika Desemba mwaka jana, ulikiuka kanuni na sheria za halmashauri, ambapo akidi ya wajumbe iliyokuwa ikihitajika kwa ajili ya meya kupigiwa kura ni madiwani tisa, lakini ni madiwani sita tu ndiyo waliopiga kura.
Katika uchaguzi huo uliohudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo, Amina Masenza (DC), pamoja na mwanasheria wa jiji la Mwanza, Savela Manzi, aliyesimamia uchaguzi huo kwa upande wa mambo ya sheria, Matata alitangazwa kuwa meya baada ya kuchaguliwa na madiwani wasiokidhi theluthi mbili.
Madiwani waliopiga kura kumchagua Matata na naibu wake (Dede Swila wa CCM), walikuwa wanne wa CCM, mmoja wa CUF ambaye ni mbunge wa viti maalumu, Mkiwa Kimwanga, na Matata mwenyewe aliyefukuzwa uanachama wa CHADEMA.
Matata alichaguliwa wakati suala lake la kufukuzwa uanachama ndani ya CHADEMA likiwa bado linangojea uamuzi wa mahakama.

Msanii Nasseeb Abdulmaliki (Diamond) atajwa sakata la "Madawa ya Kulevya"
Msanii Nasseeb Abdulmaliki (Diamond)
Kwa mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’
Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimekifikia chanzo chetu kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.
Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.
Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.
Kuhusu ziara hizo, kilicholeta mshtuko na dukuduku dhidi yake ni kuwapo kwa taarifa kwamba, katika moja ya ziara hizo za nje ya nchi, Diamond alifikia hatua ya kusafiri akitumia chumba kinachotumiwa na wageni mashuhuri (VIP), badala ya njia ya wasafiri wa kawaida.
Mbali na hilo, taarifa nyingine zinaeleza kwamba, mizigo ya msanii huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akisafiri na kundi la wacheza shoo wake, imekuwa ikipita pasipo kupitishwa katika hatua za ukaguzi kwa namna ile ile ilivyokuwa kwa mabinti wawili wa Kitanzania walionaswa nchini Afrika Kusini baada ya kuruka mfumo wa ukaguzi wa JNIA.
Aidha, ukaribu wa kimahusiano kati ya Diamond na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini na ambao majina yao pia yameanza kuhusishwa na biashara hiyo ya mihadarati, ni jambo jingine ambalo limechochea harakati za kufuatiliwa kwa karibu kwa nyendo za Diamond.
Taarifa zaidi kutoka JNIA zinaeleza kwamba, miongoni mwa watu wanaoweza wakawa wamemponza Diamond ni wale ambao walionekana kuwa karibu na Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), siku walipokuwa wakisafiri kwenda Afrika Kusini kabla hawajanaswa katika uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, wakiwa na shehena ya dawa za kulevya.
Mwenendo wa watu hao unatiliwa shaka kuwa huenda ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini, kwa sababu mbali na ukaribu na wasichana hao, pia walihusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa mwanamuziki Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kufa kwake ziligumbikwa na matumizi ya dawa za kulevya.
Alipoulizwa jana na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu taarifa hizo na iwapo amekwishahojiwa na vyombo vya dola baada ya jina lake kuanza kutajwa kuwa miongoni mwa orodha ya wasanii wa muziki wanaosafirisha dawa za kulevya, Diamond alikiri kuwa na pesa za kutosha kuishi maisha anayoyataka, lakini akakana kujihusisha na biashara hiyo.
Akifafanua tuhuma moja baada ya nyingine kwa mpangilio aliokuwa akiulizwa na gazeti hili, Diamond alisema katika maisha yake, hajawahi kujihusisha na utumiaji au usafirishaji dawa za kulevya, lakini madai hayo yamekuwa yakitolewa dhidi yake na watu ambao hawajui siri ya mafanikio yake.
“Kazi ngumu siku zote inalipa, sasa napata matunda ambayo yanatokana na kile nilichokifanya, iweje watu wanitilie mashaka, Watanzania ni mashahidi wangu wananiona navyochumia juani, nitaendelea kulia kivulini tu kwani nakula kwa jasho langu.
“Siyo kweli kwamba mizigo yangu haikukaguliwa na kama haikukaguliwa na ingekuwa na kasoro, basi Uingereza wangenitia hatiani, nilipita na nilikaguliwa.” Alisema Diamond.
Alipoulizwa kuhusu taarifa za kuwa mwanamtandao wa kundi la Masogange, pia alikanusha kwa kueleza kuwa hata siku aliyosafiri kwenda Afrika Kusini alikwenda peke yake uwanja wa ndege na kuongeza kuwa alikwenda huko kwa shughuli za kimuziki, ambapo safari nzima iligharimu zaidi ya Dola 30,000 za Kimarekani.
“Afrika Kusini nimekwenda kufanya kazi zangu na safari hiyo imenigharimu zaidi ya Dola 30,000, nilikwenda kurekodi nyimbo yangu mpya inayoitwa namba moja ambayo itaanza kusikika hivi karibuni.
“Unajua Watanzania sasa hivi wanajua mtu hawezi kufanikiwa au kupata maendeleo bila kuuza ‘unga’, hili si sawa juhudi za mtu ndizo zinamfikisha alipo, na mimi juhudi zangu ndio zinanifikisha hapa, watu waache kunijadili vibaya.” Alisema Diamond.
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja ikiwa ni takribani miezi miwili sasa tangu Watanzania wawili, Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), waliokuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya wanamuziki maarufu hapa nchini, kukamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8.
Mbali na kuwa na uhusiano wa karibu na wanamuziki, Edward anadaiwa kuwa alikuwa mfanyakazi katika mgahawa mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, unaomilikiwa na mmoja wa vijana matajiri hapa nchini ambaye hata hivyo gazeti hili halijafanikiwa kumpata ili kufanya naye mahojiano.
Wakati huo huo, tayari hatua za kinidhamu zimekwishaanza kuchukuliwa dhidi ya wafanyakazi wa JNIA waliohusika kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya, ambao Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametaja majina yao hivi karibuni na kuonyesha kwa waandishi wa habari ushahidi wa kuhusika kwao.
CHANZO: Gazeti la Mtanzania - Agosti 21, 2013

KINANA: Sina nywele kichwani kwa sababu ya kufikiria matatizo ya Watanzania!
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Ndg Abdulrahaman Kinana
"Nina uchungu na matatizo yanayowakabili watanzania na nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi na hata kukosa usingizi kwa kufikiria namna ya kukabiliana na matatizo hayo,sina hata nywele kichwani kwa sababu hiyo"
Katika mkutano huo Kinana alihutubia kwa tahadhari kubwa akiepuka kutumia maneno ambayo yangewakwaza wananchi wa Musoma.
Tofauti na ilivyozoeleka alitumia zaidi neno wapinzani na kukwepa kuitaja Chadema.
↧
Hatimaye Uchaguzi waahirishwa baada Ya CCM kukosa Wagombea!
Ni katika Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ambapo ulitangazwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika vijiji 13 na vitongoji 25 baada ya viongozi kukosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifo na kuhama vyama.
Uchaguzi ulikuwa ufanyike 13/10/2013, lakini baada ya kutangazwa na mchakato wa kuwapata wagombea kuanza na kugundulika kuwa CCM wanakosa wagombea kila mahali ndipo kikao cha dharura cha CCM wilaya kikaitishwa mkurugenzi akiwemo na kupewa agizo la kusitisha uchaguzi.
Na jana 25/09/2013 mkurugenzi alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi kwa madai kuwa halmashauri ya Sikonge haina hela ya kuendeshea uchaguzi! Kwa uchaguzi ni mpaka mwakani kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa kwa ratiba ya nchi nzima!
Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Sikonge - Tabora.

Baadhi ya watanzania ni Wanafiki na Vigeugeu!
Huu ni ukweli usio na nguo kutokana na tabia iliyojengeka na kuendelea kujengeka hata sasa kwa kusahau shida haraka, kudanganywa kwa vitu vidogo, hapa nikimaanisha kwamba unapewa starehe ya saa/siku moja tu halafu unateswa kwa miaka mitano, tunasahau matatizo yote na kumwona aliyetutesa kama hana hatia na chochote kinacho semwa juu yake ni propaganda-uongo na kumwonea.
Watanzania walio wengi tunapenda kulaumu, kutoa shutuma na kubeza harakati za vyama vya upinzani hapa nchini badala ya kujitoa kushauri na kupigania haki kwa nini kufanyike ili kusaidia kutukia kwa mambo tunayotaka.
Ukijaribu kufuatilia utagundua kwamba tulio wengi tumekuwa ni wa kwanza kuwalaumu wapinzani kana kwamba wao (Upinzani) ndio waliotutesa kwa miaka yote wakiwa madarakani na sasa ameingia msamaria mwema Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kukusaidia.
Wananchi tusibweteke na ukaribu tunaoonyeshwa sasa hivi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na badala yake tujiulize ni kwanini sasa na si hapo kabla?! Hii yote ni danganya toto kwasababu chaguzi zimekaribia na hayo mnayoyaona ni machozi ya mamba.
Tusijitie upofu kwenye matatizo yetu bali tujifunze kutokana na matatizo yaliyotupata
Baadhi yetu tukiacha tabia hizi tutafka tunapopataka.
Huu ni ushauri kutoka kwa mmoja kati ya wasomaji wa blog hii.
↧
↧
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani aanguka Chooni kwa mgaga wa Kienyeji na kufariki!
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani, Kimara King’ong’o jijini Dar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni kiongozi wa umoja wa wazazi, Seleman Hashim Ndege amefariki dunia nyumbani kwa mganga wa kienyeji ‘Sangoma’, Veronica Kasumen ‘mama Misingo’ na kifo chake kuacha utata, Ijumaa lina habari kamili.
Akizungumza kwa uchungu mke wa marehemu, Mwajuma Ally amesema kuwa siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) mume wake aliamka asubuhi saa 12 na kwenda kusambaza vipeperushi vya kazi zake za serikali ya mtaa.
Mwajuma alisema ilipotimu saa tisa alasiri, alifuatwa na mama Misingo na kumwambia kuwa mume wake amefariki dunia nyumbani kwake na kumtaka waende kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Tumbi, Kibaha.
“Nilishtuka sana kwa kuwa mume wangu hakuwa akiumwa chochote, niliambatana na mama Misingo kwenda nyumbani kwake,” alisema Mwajuma kwa unyonge.
Mke huyo aliendelea kudai kwamba alipotoka nje alikutana na gari la Kituo cha Polisi cha Mbezi Kwa Yusuf waliomwamuru kuingia ndani ya gari hilo aina ya Land Rover ‘Difenda’ huku wakimuuliza kama amemuona mume wake.
“Kilichonishtua ndani ya gari kulikuwa na wanaume wengine wawili wakanionesha mwili wa mume wangu ukiwa tayari umeshavalisha sanda bila ya kunishirikisha,” aliendelea kusema Mwajuma...
Mke huyo alisema kuwa alimhoji mama Misingo kilichotokea, naye akamwambia kuwa mumewe alifika kwake kwa lengo la kumuona mtoto wake ambaye alianguka na pikipiki lakini ghafla akaanguka na kuaga dunia mara baada ya kuomba kuingia msalani.
“Tulienda mpaka Hospitali ya Tumbi ambapo mwili ulihifadhiwa kisha tukarudi nyumbani,” alimaliza mke wa marehemu huku akisema kuwa amebaki na utata juu ya kifo cha mumewe.
Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani ambapo marehemu alikuwa akiishi, Fadhili Mzee Jakaya alisema alishtushwa na taarifa za kifo hicho na kuzifuatilia.
“Mimi na wenzangu tulienda Kituo cha Polisi cha Mbezi lakini tulishangaa kukuta mganga huyo (mama Misingo) ameandikisha kuwa ni mkazi wa Kibamba na aliyefariki ni kaka yake aliyefika nyumbani kwake kumuona mpwa wake ndipo alipoanguka chooni, hicho kilitushangaza,” alisema.
Jakaya alisema kitendo cha mganga huyo kudanganya eneo analoishi na udugu wake na marehemu kiliwafanya waamini kuwa kulikuwa na kitu nyuma ya pazia.
“Tunasikia Ndege alifariki saa tatu asubuhi, imekuwaje wamekaa naye hadi saa tisa jioni, haya kama si maajabu ni nini? Pia kwa nini wamvalishe sanda? Hapa kuna sababu zitajulikana tu,” alisema Jakaya.
Wananchi wa Michungwani walijikusanya na kwenda nyumbani kwa mama Misingo na kumkuta akiwa na mumewe ambapo walimhoji kuhusu maelezo tata aliyoyatoa kituo cha polisi.
Hata hivyo, viongozi wa serikali ya mtaa walitoa taarifa polisi ambao walifika nyumbani kwa mganga huyo baada ya nusu saa na kuondoka naye.
Habari zilizopatikana kutoka kwa majirani zinadai Ndege alifika nyumbani kwa mama Misingo na kutibiwa kwa kupewa dawa lakini cha ajabu akafariki dunia.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo anapoishi mama Misingo, Demetrius Mapesi amesikitishwa na kitendo hicho na kusema iwapo vipimo vitabaini kuwa dawa aliyokunywa marehemu ni sumu watachukua hatua kali.
Waandishi wetu walifika nyumbani kwa mama Misingo na kuzungumza na watoto wake, ambapo mmoja wao alisema kuwa, marehemu alifika nyumbani kwao saa tatu asubuhi kwa lengo la kumuona kaka yao aitwaye George ambaye alikuwa mgonjwa.
“Baada ya muda aliomba kwenda chooni na kukaa huko kwa muda mrefu, mama akamsikia akikoroma ndipo akaniambia nivunje mlango nimtoe.
“Nilifanya hivyo, tulikuwa na mama na mzee mmoja (jina linahifadhiwa) tulijaribu kumvua nguo na kumwagia maji lakini alikuwa tayari ameshafariki dunia, mama akapiga simu kuwaita polisi,” alisema mtoto huyo.
Naye jirani mwingine wa mama Misingo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema hawakupewa taarifa za mtu kuanguka chooni na alipoliona gari la polisi limewabeba alihoji na kuambiwa kuwa hakukuwa na tatizo lolote.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Tumbi, mwili wa marehemu uliagwa nyumbani kwake Kimara Michungwani kisha kusafirishwa kwenda Mtwara kwa ajili ya mazishi ambapo mtaani vilio vilitawala kila kona wakati wa kuuaga mwili.
Bado wakazi wa Kimara Michungwani wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua kilichosababisha kifo cha Ndege.
Chanzo JF
↧
News Alert: Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania yafungiwa!
Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI
2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya
habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya
habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari
yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika
maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la
ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya
kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya
Habari.
Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwaujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya
wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa
haviwasaidii.
wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa
haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,. Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA, 2013
↧
Hotuba ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete kwa wananchi, Tarehe 4 Octoba 2013
Ndugu Wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza mwezi Septemba salama na kuwasiliana kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri. Naomba radhi kuzungumza nanyi siku ya leo kwa sababu nilikuwa safari na nilirejea jioni ya tarehe 30 Septemba, 2013. Awali nilifikiria nisiseme, nisubiri mwisho wa mwezi wa Oktoba. Lakini, baada ya kupata taarifa ya yaliyojiri, nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia. Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno. Nitayatafutia mahali pengine pa kuyasemea.
Uhusiano na Rwanda
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Julai, nilizungumzia hali ya uhusiano wetu na Rwanda kutokuwa mzuri na tatizo la ujambazi na wahamiaji haramu katika Mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera. Nafurahi kusema kuwa kwa yote mawili kuna maendeleo ya kutia moyo.
Tarehe 5 Septemba, 2013, nilikutana na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Paul Kagame wa Rwanda mjiniKampala . Tuliitumia fursa ya ushiriki wetu katika Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia uhusiano baina yetu na nchi zetu. Mazungumzo yalikuwa mazuri na sote tulikubaliana kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Kwa sababu hiyo tulielewana kuwa tutengeneze mazingira yatakayosaidia kutuliza hali na kurudisha nchi zetu katika uhusiano mwema kama ilivyokuwa siku zote. Nawaomba ndugu zangu hususan wanasiasa, watumishi wa umma, wanahabari na wenye mitandao ya kijamii na blog na wananchi kwa ujumla tusaidie kuimarisha uhusiano mwema baina ya Rwanda na Tanzania na watu wake.
Majambazi na Wahamiaji Haramu
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba hiyo pia nilisema kuwa tutachukua hatua thabiti dhidi ya majambazi na wageni wanaoishi nchini bila ya kuzingatia taratibu zinazohusika. Niliwataka majambazi wajisalimishe wao na silaha zao kwa hiari. Wale wanaoishi nchini bila ya kuwa na kibali halali wahalalishe ukaazi wao au warejee makwao. Nilitoa siku 14 kuanzia tarehe 29 Agosti, 2013 wafanye hivyo kwani baada ya hapo tungeanzisha operesheni maalum ya kushughulika na watu wa makundi yote mawili.
Ndugu Wananchi;
Kumekuwepo na mafanikio ya kutia moyo. Kwa upande wa wahamiaji wanaoishi nchini kinyume cha sheria watu wapatao 21,254 waliondoka kwa hiari. Hali kadhalika zaidi ya ng’ombe 8,000 waliondolewa na silaha 102zilisalimishwa. Baada ya operesheni kuanza tarehe 6 Septemba, 2013 na kumalizika tarehe 20 Septemba, 2013, wahamiaji haramu 12,828 walirejeshwa makwao na watuhumiwa 279 wa unyang’anyi wa kutumia silaha walikamatwa. Aidha, mabomu 10 ya kutupa kwa mkono (offensive hand grenades), silaha 80, risasi 780 na mitambo 2ya kutengeneza magobole vilikamatwa. Pia, ng’ombe 8,226walikamatwa wakichungwa katika mapori ya hifadhi. Kwa upande wa mazao ya misitu, mbao 2,105 zilikamatwa pamoja na nyara mbalimbali za Serikali.
Ndugu Wananchi;
Agizo la kuwataka watu wanaoishi nchini isivyo halali wahalalishe ukaazi wao au waondoke kwa hiari au wataondolewa lilipotoshwa hasa na vyombo vya habari vya nje ya Tanzania. Walikuwa wanadai eti Tanzania ilikuwa inafukuza wakimbizi. Madai hayo si ya kweli hata kidogo. Hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2013 wakimbizi 68,711walikuwepo kwenye Kambi ya Nyarugusu, Mkoani Kigoma. Hakuna mkimbizi ye yote aliyetakiwa kuondoka. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ye yote kati ya wale watu walioondoka kwa hiari au kusaidiwa kuondoka wakati wa operesheni ambaye ni mkimbizi. Kama ingekuwa hivyo, wa kwanza kulalamika wangekuwa wenzetu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Bahati nzuri jambo hilo halikutokea.
Ndugu Wananchi;
Yalikuwepo pia madai kwamba tunawaonea na kuwatesa watu walioishi nchini miaka mingi. Ati iweje sasa ndiyo waambiwe kuwa siyo raia. Siku zote Serikali ilikuwa wapi? Uraia haupatikani kwa kuishi nchi ya kigeni kwa miaka mingi. Unapatikana kwa kutimiza masharti ya kuomba na kupewa uraia. Kama mtu hakufanya hivyo anabaki kuwa raia wa nchi aliyotoka au walikotoka wazazi wake. Ipo mifano ya watu mashuhuri ambao walilazimika kuachia nyadhifa zao baada ya kugundulika kuwa siyo raia. Hawakuwa wanaonewa, ndiyo matakwa ya Katiba na Sheria za nchi yetu.
Ndugu Wananchi;
Katika kutekeleza operesheni hii niliagiza kuwa wale watu ambao wameishi hapa nchini miaka mingi ambao wana nyumba, mashamba au mali mbalimbali au wameoa au kuolewa na wana watoto au hata wajukuu waelekezwe kuhalalisha ukaazi wao. Iwapo watakataa kufanya hivyo basi wasaidiwe kurejea kwao. Pia niliagiza watu wasiporwe mali zao wala kudhulumiwa. Sijapata taarifa ya kufanyika kinyume na maelekezo yangu. Lakini kama wapo watu waliotendewa tofauti, taarifa itolewe kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa au hata Ofisi ya Rais ili hatua zipasazo zichukuliwe. Hatutaki watu wadhulumiwe au kuonewa.
Napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Waziri wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi kwa uongozi wao mzuri katika zoezi hili. Pia, nawapongeza Makamanda na askari wa JWTZ na Polisi pamoja na maafisa wa Idara ya Uhamiaji, Idara ya Mifugo, Idara ya Wanyamapori, Idara ya Misitu na Idara nyinginezo za Serikali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Najua awamu ya kwanza imeisha tarehe 20 Septemba, 2013 na kama nilivyosema kuwa safari hii operesheni itakuwa endelevu, muda si mrefu awamu ya pili itafuata. Nawaomba waendelee kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu ya hali ya juu.
Ziara ya Canada na Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 17 na 28 Septemba, 2013 nilifanya ziara ya kikazi katika nchi za Canada na Marekani. Nchini Canada nilitembelea Chuo Kikuu cha Guelph ambapo nilitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua jitihada zetu tuzifanyazo kujiletea maendeleo na mafanikio ya kutia moyo tunayoendelea kupata licha ya changamoto zinazotukabili. Katika mazungumzo yangu na uongozi wa chuo hicho wamekubali kuwa na ushirikiano wa karibu na Wizara zinazohusika na Elimu, Kilimo na Mifugo pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma. Nimewataka Mawaziri wa Wizara hizo na viongozi wa vyuo hivyo kuchangamkia fursa hiyo bila kuchelewa.
Ndugu Wananchi;
Nchini Marekani nilikutana na kuzungumza na maafisa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya nchi hiyo wakiwemo Rais Barack Obama na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Marekani. Mazungumzo yetu yalilenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zetu na mambo yalienda vizuri. Wote walituhakikishia kuwa mambo tuliyoyazungumza na kukubaliana na Rais Barack Obama wakati wa ziara yake nchini yanaendelea kufanyiwa kazi. Miongoni mwa hayo maombi yetu ya kupatiwa vitabumilioni 2.4 vya sayansi na hisabati yamekubaliwa na utekelezaji umeanza. Upatikanaji wa vitabu hivyo utamwezesha kila mwanafunzi wa sekondari kuwa na kitabu chake.
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na la faraja kwetu ni kuwa mapendekezo yetu ya miradi ya umeme na barabara za vijijini za kugharamiwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lao la Changamoto za Milenia yamepokelewa vizuri. Kinachosubiriwa ni miradi ipi itakubaliwa na Bodi ya MCC na kiasi gani cha fedha kitatengwa na Bunge la Marekani kwa ajili hiyo.
Tuzo ya Uhifadhi
Jambo lingine muhimu katika safari yangu ya Marekani ni kutunukiwa tuzo na “International Congressional Conservation Foundation” kwa kutambua juhudi zetu katika kuhifadhi wanyama pori na mafanikio tuliyoyapata. Licha ya changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, tuzo hii imetupa moyo wa kuongeza nguvu katika jitihada tunazozifanya sasa kupambana na ujangili na matatizo mengine ya uhifadhi wa wanyama na misitu.
Ndugu Wananchi;
Kilichotupa moyo zaidi ni kauli za utayari wa kutusaidia katika mapambano hayo zilizotolewa wakati wa kupewa tuzo na katika mkutano wa mfuko wa Maendeleo wa Clinton na katika mkutano maalum wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo duniani.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ndugu Wananchi;
Shabaha kuu ya safari yangu ya Marekani ilikuwa kuhudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York mpaka Desemba, 2013. Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni kuandaa agenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yaani: Post 2015 Development Agenda: Setting the Stage. Kama mtakavyokumbuka Malengo ya Milenia yaliyoamuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, yanafikia ukomo wa utekelezaji wake mwaka 2015.
Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu mjadala umehusu nini kifanyike baada ya mwaka 2015. Hata hivyo, mjadala huo unaanza kwa kufanya tathmini ya utekelezaji wa yale Malengo Manane ya Milenia ya mwaka 2000 umefikia wapi mpaka sasa na utafikia wapi mwaka 2015 kwa kila nchi na kwa dunia kwa ujumla. Tathmini ya jumla inaonesha kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa ya kutekeleza malengo haya katika kila nchi. Yapo malengo ambayo utekelezaji wake umefikia shabaha hivi sasa na yapo ambayo upo uwezekano wa shabaha kufikiwa ifikapo mwaka 2015. Vile vile yapo ambayo shabaha haitafikiwa.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wetu, Tanzania, tumefikia shabaha katika mambo yafuatayo:
(1) Lengo la Milenia namba 2 kuhusu uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule ya msingi;
(2) Lengo la Milenia namba 3 hasa kuhusu usawa wa kijinsia katika Shule za Msingi na Sekondari. Ukweli ni kwamba, wasichana wanaanza kuwa wengi kuliko wavulana. Hatujafikia shabaha kwa upande wa usawa wa kijinsia katika elimu ya juu na ni vigumu kulifikia ifikapo 2015. Pia hatujafikia lengo kwa upande wa usawa wa Wabunge wanawake na wanaume. Hata hivyo, kwa kutumia mchakato wa Katiba unaoendelea sasa tunaweza kufikia lengo katika uchaguzi wa 2015 iwapo tutaamua iwe hivyo;
(3) Lengo la Milenia namba 4 kuhusu kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano;
(4) Tumefikia shabaha kwa Lengo la Milenia Namba 6 kuhusu kupunguza maambukizi ya UKIMWI; na
(5) Kwa upande wa lengo namba 7 kuhusu mazingira, tumefikia shabaha kwa upande wa upatikanaji wa maji mijini. Bado tuko nyuma kwa maji vijijini ingawaje tunaweza kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 kama tutaendeleza uwekezaji tulioamua kufanya katika bajeti ya mwaka huu. Lakini, hatutaweza kufikia shabaha kwa upande wa usafi wa mazingira mijini na vijijini ifikapo mwaka 2015. Safari bado ndefu sana.
Ndugu Wananchi;
Malengo ya Milenia namba 1 na namba 5 ambayo bado tuko nyuma sana ya shabaha hatutafikia lengo ifikapo 2015. Tumeendelea kutekeleza lengo la Milenia namba 1kuhusu kupunguza umaskini na njaa kwa zaidi ya nusu kutoka kiwango cha mwaka 2000. Hatua tunazochukua kuleta mageuzi katika kilimo zina lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza mapato ya wakulima. Mafanikio yanaanza kuonekana lakini si ya kiwango cha kutufikisha kwenye lengo ifikapo mwaka 2015. Tunao, pia, mpango wa kupanua programu ya TASAF ya Conditional Cash Transfer ili tuwafikie watu wengi maskini. Hata kama tutafanikiwa kuutekeleza mapema mpango huu utatusogeza sana mbele lakini bado tutakuwa chini ya lengo kwa upande wa kupunguza umaskini ifikapo 2015.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Lengo la Milenia namba 5, kuhusu afya ya kina mama wajawazito bado tuko nyuma katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na kuongeza idadi ya wajawazito wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Hatutaweza kufikia shabaha ifikapo mwaka 2015. Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (2007 – 2017) una nia ya kukabiliana na matatizo haya. Tumeongeza ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali, tumeboresha upatikanaji wa dawa na tumepanua sana mafunzo ya madaktari, wauguzi na wakunga mambo ambayo yamesaidia kutufikisha hatua tuliyopiga mpaka sasa. Naamini juhudi zetu tukiziendeleza zitatusogeza mbele zaidi ingawaje bado tutakuwa chini ya lengo. Miaka michache ijayo, tatizo hili nalo litakuwa historia.
Ndugu Wananchi;
Lengo la Milenia namba 8 linazihusu nchi tajiri kuongeza michango yao kusaidia nchi zinazoendelea kutekeleza Malengo ya Milenia. Bahati mbaya sana mataifa tajiri hayajafikia viwango wanavyotarajiwa kutoa na hata vile wanavyoahidi wenyewe kutoa katika majukwaa mbalimbali. Kama wangetimiza ahadi zao, sura ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia ingekuwa tofauti kabisa.
Ndugu Wananchi;
Hiyo ndiyo hali ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia hapa nchini. Hakuna nchi ye yote duniani iliyofanikiwa kutekeleza shabaha za malengo yote kwa ukamilifu. Ushauri wa viongozi wote waliozungumza ulitaka mataifa yaliyoendelea yatimize ahadi zao za kuchangia utekelezaji wa Malengo ya Milenia. Ilionekana suala la upatikanaji wa fedha halina budi kuangaliwa kwa makini sasa na baada ya mwaka 2015. Bila ya hivyo ufanisi utakuwa mdogo katika kuongeza kasi ya utekelezaji kwa pale paliposalia kufikia malengo ya 2015 na hata kwa Malengo ya baada ya mwaka 2015.
Mashambulizi ya Kigaidi ya Westgate, Nairobi
Ndugu Wananchi;
Wakati nikiwa safarini, tarehe 21 Septemba, 2013 kulitokea shambulilizi la kigaidi katika Jengo la Biashara la Westgate, huko Nairobi, Kenya. Watu 67 walipoteza maisha na zaidi ya 200 walijeruhiwa. Nilituma salamu za pole na rambirambi kwa Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wa Kenya na kuwahakikishia kuwa tupo pamoja nao katika wakati huu wa majonzi.
Nafahamu kuwa baada ya tukio hilo watu wengi hapa nchini wameingiwa na hofu kuhusu usalama wetu. Ni hofu ya msingi kwani tarehe 8 Agosti, 1998 Ubalozi wa Marekani hapa nchini ulishambuliwa na magaidi na ndugu zetu 11wasio na hatia walipoteza maisha.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwafahamisha kuwa tangu shambulio la mwaka 1998, Serikali imekuwa inajenga uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kupambana na ugaidi katika nyanja mbalimbali. Tunaendelea kujiimarisha bila kusita siku hadi siku. JWTZ, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa ajili hiyo. Juhudi zetu hizo ndizo zinazotufanya tuwe salama hadi sasa.
Baada ya tukio la Kenya, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeimarisha mikakati yao maradufu. Pamoja na kujizatiti kwetu huko hatuwezi kusema kuwa tukio la kigaidi halitaweza kutokea nchini. Uhakika huo hatuna kwani hata mataifa makubwa na tajiri yameshambuliwa. Kilicho muhimu ni kuendelea kuchukua tahadhari na wananchi kusaidia ili vyombo vyetu vifanikiwe zaidi.
Hali kadhalika, tumewataka watu wote wenye shughuli zinazokusanya watu wengi kama vile maduka, maofisi, mahoteli, migahawa n.k. waweke kamera za ulinzi nje na ndani ya maeneo yao. Pia waangalie uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi (metal detectors and x-rays). Najua watu wanaweza kulalamikia usumbufu au gharama, lakini gharama na hasara ya kushambuliwa ni kubwa zaidi kuliko ya usumbufu huo.
Ndugu Wananchi;
Nawaomba muendelee kufanya shughuli zenu bila ya hofu ingawaje msiache kuwa makini na kuchukua tahadhari. Watu watoe taarifa kwa vyombo vya usalama wanapoona mtu au watu au kitu cha kutilia shaka. Ni muhimu kwa usalama wake, wa kila mtu, jamii na taifa. Maafisa husika wa vyombo vya ulinzi na usalama wataendelea kuelimisha umma kuhusu hatua mbalimbali za tahadhari za kuchukua. Sisi Serikalini tumejipanga kuchukua hatua zaidi kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu na watu wake.
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wananchi;
Baada ya Bunge la Novemba, 2011 kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kulikuwepo na madai ya kutaka sheria hiyo iboreshwe kutoka vyama vyote vya siasa vikiwemo vyama vya upinzani na Chama tawala. Majadiliano yalifanyika baina ya Serikali na vyama hivyo pamoja na shirikisho la asasi za kiraia. Makubaliano yalifikiwa kuwa marekebisho yafanyike kwa awamu. Awamu ya kwanza ihusishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba kisha hapo yafanyike marekebisho yanayohusu Bunge Maalum na mwisho Kura ya Maoni.
Kama ilivyokuwa kwa mabadiliko yaliyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba, safari hii nayo vyama vya siasa vilitoa mapendekezo yao. Yalifanyika mazungumzo kati yao na Serikali na maelewano kufikiwa kuhusu maeneo ya kufanyiwa marekebisho. Serikali ilitayarisha rasimu ya Muswada na kuuwasilisha kwa wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ndugu Wananchi;
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa mapendekezo yake na ushauri kwenye maeneo mawili. Kwanza kwamba uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum ufanywe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kuafikiana na Rais wa Zanzibar. Pili walishauri kwambakama Bunge Maalum litashindwa kufikia maamuzi ndani ya siku 70 zilizopendekezwa, liweze kuongezwa muda hadi kufikia siku 90. Maeneo mengine ya Muswada waliafikiana nayo.
Ndugu Wananchi;
Kwa kuzingatia utaratibu wa kutunga Sheria, Serikali ilifikisha Muswada kwa Spika wa Bunge ambaye nae aliuwasilisha kwenye Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala. Kama ilivyo ada, Kamati hiyo ilifanya vikao na wadau na kupokea maoni yao kuhusu Muswada. Nimeambiwa kulikuwa na mjadala wa kina na mapendekezo mazuri yalitolewa na wadau. Kisha hapo Wajumbe wa Kamati walikaa wenyewe kujadili Muswada walikuwepo pia Wabunge ambao si Wajumbe wa Kamati walioshiriki kwa vile Kanuni zinaruhusu. Nimeambiwa pia kwamba mjadala ulikuwa mpana na wa kina zaidi. Mapendekezo kadhaa yalitolewa na Wajumbe kuhusu vifungu mbalimbali vya Muswada.
Ndugu Wananchi;
Nimefahamishwa kuwa Wabunge wa vyama vyote walichangia na kwamba baadhi ya nyakati mambo yalipokuwa ugumu mawazo mazuri ya baadhi ya Wabunge wa upinzani yalisaidia kupata ufumbuzi. Nimeambiwa pia kwamba Wajumbe wa Kamati na upande wa Serikali walikubaliana kwa maeneo mengi isipokuwa machache ambayo walikubaliana kwa pamoja wayapeleke Bungeni ili Wabunge nao wayajadili na kuyapatia ufumbuzi.
Ndugu Wananchi;
Baada ya Kamati kumaliza kazi yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mathias Chikawe aliwasilisha Muswada Bungeni. Akafuatiwa na Mheshimiwa Gosbert Blandes kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kutoa maoni ya Kamati. Baadaye Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake.
Ndugu Zangu;
Baada ya watu hao watatu kutoa maoni yao ilitarajiwa kuwa Wabunge wangeanza kujadili Muswada. Naambiwa mambo hayakuwa hivyo. Badala yake kukazuka malumbano baina ya Spika na baadhi ya Wabunge wa Upinzani wakitaka Muswada usijadiliwe. Ilifikia wakati hoja hiyo ikabidi iamuliwe kwa kura ambapo ilishindwa. Katika hali isiyotarajiwa, Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje ya Bunge isipokuwa wawili. Kitendo hicho kimewanyima Wabunge wengi wa upinzani fursa ya kutetea hoja zao walizozitoa kupitia hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani. Pia wamejinyima nafasi ya kusema mambo mengine wakati wa mjadala na Kamati ya Bunge zima.
Wabunge waliokuwepo waliendelea kuujadili Muswada na kutoa hoja na mapendekezo ya kuuboresha. Walifanya hivyo wakati wa mjadala na wakati wa kupitia kifungu kwa kifungu. Baadhi ya hoja na mapendekezo yalikubaliwa na mengine yalikataliwa. Miongoni mwa yaliyokubaliwa na Wabunge, kwa mfano, ni kuhusu elimu ya mtu atakayekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum na lile la ukomo wa uhai wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
Kwa maoni yangu madai ya Kambi ya Upinzani yanazungumzika na hata baadhi yangeweza kukubalika kama Wabunge wake wangekuwepo Bungeni na kushiriki mchakato wote wa kujadili na kupitisha Miswada Bungeni. Bahati mbaya hawakuwepo, hivyo hapakuwepo na mtu wa kusema mawazo yao. Baada ya kupoteza fursa yao halali, kutaka kupata ufumbuzi nje ya Bunge ni jambo lisilowezekana. Haya ni masuala yanayohusu Bunge ambayo hujadiliwa na kuamuliwa Bungeni na si vinginevyo. Kuandamana nchi nzima au kuchukua hatua za kutotii sheria kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Freeman Mbowe anavyotaka, hakutaleta mabadiliko wanayoyataka katika sheria hii. Naamini na wao wanautambua ukweli huo.
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo wa wahenga kuwa “historia hujirudia”. Naomba hekima ziwaongoze viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na zituongoze sote kutumia utaratibu tulioutumia mwaka 2012. Kulipotokea mazingira kama haya pande zote zilikaa pamoja na kuzungumzia hoja moja baada ya nyingine na kukubaliana nini kifanyike na kifanyike vipi. Baada ya kuridhiana hatua zipasazo za kisheria na kanuni zilichukuliwa na kumaliza mzozo.
Ndugu Wananchi;
Kufanya kinyume cha hayo hakutaleta ufumbuzi wa mzozo huu. Tutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima. Tukikataa kufanya hayo Watanzania wanayo kila sababu ya kuhoji dhamira zetu na kutilia shaka nia zetu. Watakuwa na haki ya kuuliza nia ni hii yetu sote ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia njia za kikatiba na kisheria au tuna dhamira nyingine iliyojificha?
Kama dhamira yetu ni kutaka kupata Katiba mpya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ushauri wangu na rai kwa ndugu zetu wa CHADEMA, CUF na NCCR-Maguezi ni kuwa waachane na mipango ya maandamano na kufanya ghasia. Badala yake watumie njia halali zinazotambulika kikatiba na kisheria kujenga hoja za kufanya marekebisho wanayoyaona wao yanafaa kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Tukifanya hivyo tutakuwa tunajenga badala ya kubomoa. Tutaliponya taifa. Sisi katika Serikali tuko tayari.
Ndugu Wananchi;
Napenda pia kuzisemea baadhi ya hoja zilizotolewa na Kambi ya Upinzani. Kwanza kabisa nasema kuwa nimesikitishwa sana na madai na tuhuma za uongo eti katika uteuzi wa Tume ya Katiba sikuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu. Nasema hivyo kwa sababu, sipendi kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amesema yale kwa kutokufahamu ukweli au kwa bahati mbaya. Amesema yale kwa makusudi mazima ya kupotosha ukweli ili pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue waleWajumbe 166 wa Bunge Maalum.
Napenda ieleweke kuwa siishabikii kazi hiyo, lakini kwa kutimiza wajibu na maslahi ya taifa nikiagizwa na Sheria za nchi nitafanya. Nasema hivyo kwa sababu nafahamu ni kazi ngumu. Kama kazi ya uteuzi wa Wajumbe 30 wa Tume haikuwa rahisi hata kidogo, hii ya uteuzi wa watu 166 itakuwa ngumu zaidi. Ile ya Tume ilikuwa ngumu kwa namna mbili. Kwanza, kwamba taasisi zilizoomba na waombaji walikuwa wengi mno kuliko nafasi za kujaza yaani 15 Zanzibar na 15 Bara. Zanzibar ziliomba taasisi zaidi ya 60 na waombaji walikuwa zaidi ya 200 wakati Bara kulikuwa na taasisi zaidi ya 170 zikiwa na waombaji zaidi ya 500. Kupata watu 30 kutoka orodha kubwa kiasi hicho si mtihani mdogo. Pili kwamba tulitakiwa kuunda Tume inayoasili sura ya taifa, yaani watu wa nchi yetu kwa maeneo, vyama vya siasa, dini, wanawake, vijana, walemavu, wafanyakazi, wasomi, Wabunge, Wawakilishi, wanasheria, wafanyabiashara, wakulima, asasi za kiraia n.k.
Ndugu Wananchi;
Pamoja na changamoto hizo, lakini tulifanikiwa kuunda Tume iliyopokelewa vizuri na jamii na kufanya watu wengi hata wale ambao hawakuteuliwa wahisi kuwakilishwa. Tulifanyaje? Kwanza kabisa tulihakikisha kuwa tunapata wawakilishi wa vyama vya siasa vyenye wawakilishi Bungeni na kwenye Baraza la Wawakilishi na tunapata wawakilishi wa mashirika ya dini zetu kubwa yaani, TEC, CCT na BAKWATA. Ndiyo maana nikasema kuwa kwa Mheshimiwa Tundu Lisu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu.
Baada ya hapo ndipo tukaangalia waombaji wa makundi na taasisi nyingine. Tulijitahidi sana kupata watu ambao wanawakilisha kundi zaidi ya moja. Tulifikiria hivyo kwa sababu ni ukweli ulio wazi kuwa si kila taasisi iliyoomba itapata mwakilishi kwani hata tungependa iwe hivyo nafasi hazikuwepo. Kwa kutumia utaratibu huu makundi mengi yamepata uwakilishi kutokana na watu waliopendekezwa na makundi mengi. Tumefanya kazi kubwa sana ya kuwianisha mambo na makundi ya maslahi mbalimbali nchini.
Ndiyo maana naiona mantiki ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Rais wa Zanzibar wa kuwateua Wajumbe wa Bunge Maalum. Dhana kuwa kila kikundi kiteue chenyewe watu ingefaa sana kama kungekuwepo na nafasi za kutosha kila kundi nchini. Hilo haliwezekani, labda tuwe na Bunge Maalum lisilokuwa na ukomo wa wajumbe.
Ndugu Wananchi;
Mimi na Rais wa Zanzibar tumekuwa tunajiuliza baada ya kazi ngumu na nzuri tuliyoifanya na iliyopongezwa na wengi ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba nini kilichoharibika sasa hata tuonekane hatuaminiki kuteua hawa 166? Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu, nimeshasema hazina ukweli wowote. Ninapojiuliza kwa nini aseme uongo nashindwa kupata jibu linaloingia akilini. Wakati mwingine nafikiria kuwa ni hiana. Lakini nadhani ni hila za kisiasa zenye nia ya kutaka kupata watu wa kutetea maslahi ya chama chake. Kama hiyo ndiyo shabaha basi amekosea sana.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Hatutengenezi Katiba ya Chama fulani bali Katiba ya nchi, Katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama ambao ndiyo wengi kuliko wote. Lazima tuongozwe na ukweli huo na tuwe na msimamo huo wakati wote. Lazima tukumbuke kuwa si watu wote wanaostahili au kuwa na sifa ambao wataomba na kupata nafasi ya kuwa Wajumbe, hivyo wale wachache watakao bahatika lazima wawasemee wote. Wanatakiwa kusikiliza na kuwakilisha mawazo ya wote hata wale wasiokuwa wa Chama chao au kundi lao.
Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri hii ndiyo sifa kubwa iliyooneshwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wamewasimamia na kuwasemea watu wote bila ya kubagua. Natambua kuwepo kwa baadhi ya watu ambao hawafurahii msimamo huo na matokeo ya kazi yao. Watu hao kuwalaumu Wajumbe wa Tume kwa ajili hiyo ni kuwaonea na kutowatendea haki. Tunataka watakaokuwa Wajumbe wa Bunge Maalum nao waige mfano huu mzuri. Wajali maslahi mapana ya taifa letu na watu wake badala ya kujali yale ya taasisi zao au makundi yao .
Ndugu Wanachi;
Nimeambiwa pia kuliwepo madai ya Zanzibar kutokushirikishwa ipasavyo. Nimeeleza kwa kiasi gani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshirikishwa na kutoa maoni yake yaliyojumuishwa katika Muswada. Hivyo basi napata tabu kuyaelewa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa msingi wake nini! Labda kuna kitu sikuambiwa!
Nimeulizia kuhusu hoja ya Kamati kutokufanya vikao Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau wa Zanzibar. Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati haistahili kulaumiwa. Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulauminiana isivyostahili. Hivyo basi, kuligeuza jambo hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya maandamano sidhani kama ni sawa.
Ndugu Wananchi;
Nimeambiwa pia kuwa kulikuwa na hoja ya kutaka idadi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar iwe sawa kama ilivyo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sababu ya idadi ya Wajumbe wa Tume kuwa sawa inatokana na utaratibu wao wa kufikia uamuzi. Ni kwa maelewano ya wote (consensus) na siyo kwa kupiga kura. Ndiyo maana idadi imewekwa sawa ili sauti za pande zote zisikike sawia. Bunge Maalum lina sharti la kufanya uamuzi kwa theluthi mbili ya kura za kila upande kukubali. Bila ya hivyo hakuna uamuzi.
Hivyo basi, katika Bunge Maalum nguvu si uwingi wa kura ambazo upande fulani unaweza kupata bali ni ulinganifu sawa wa kura za kila upande peke yake. Huu ndiyo msingi unaotumika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa kwa lengo la kulinda maslahi ya Zanzibar. Zanzibar ina Majimbo 50 ya uchaguzi na Tanzania Bara ina Majimbo 189, hivyo ukiamua kwa wingi kila wakati Wazanzibari watashindwa. Lakini, hapajakuwepo madai ya Zanzibar nao kutaka kuwa na idadi sawa ya majimbo kama Bara au kupunguza majimbo ya Bara yawe sawa na ya Zanzibar kwa sababu wingi si hoja. Msingi unaotumika ni kutoa nguvu sawa za uamuzi kwa kila upande wa Muungano wakati wa kuamua masuala ya Katiba. Hakuna mdogo wala mkubwa, wote wako sawa. Hakuna mdogo kumezwa na mkubwa. Ndiyo msingi unaopendekezwa kutumika kwenye Bunge Maalum hivyo hakuna kitakachoharibika kwa idadi ya Wajumbe kutokukulingana. Nadhani inafaa ibaki ilivyo. Lakini kama Wabunge wataamua waongeze idadi itakuwa kwa sababu nyingine siyo hii ya mfano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
Katika orodha ya madai ya ndugu zetu wa upinzani lipo suala la uhai wa Tume ya Katiba. Wanataka usiishe wanapokabidhi rasimu ya pili kwa Bunge Maalum bali waendelee kuwepo mpaka mwisho wa mchakato. Nimeulizia ilikuwaje? Nimeelezwa kuwa jambo hili halitokani na mapendekezo ya Serikali wala ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala. Limetokana na pendekezo la Mbunge katika Bunge wakati wa kupitia vifungu na kuungwa mkono na Wabunge wengi. Kwa hiyo kuilaumu Serikali si haki. Serikali inaweza kuwa mshirika katika hoja hii.
Nami naiona hoja ya Wajumbe wa Tume kuwa na wajibu wakati wa Bunge Maalum hasa wa kusaidia kufafanua mapendekezo ya Tume. Je ushiriki huo uwe vipi? Je ni Wajumbe wote au baadhi yao ni jambo linaloweza kujadiliwa.
Ndugu Wananchi;
Naomba nimalizie kwa kuwasihi viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kuongozwa na hekima iliyotumika wakati tulipokuwa na tatizo linalofana na hili kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mimi naamini kama iliwezekana kufanikisha mambo wakati ule inaweza kufanya hivyo hata safari hii. Itatufikisha pale tunapopataka salama salimini bila maandamano, kushupaliana au uvunjifu wa amani. Kupanga ni kuchagua, naomba sote, mmoja mmoja na kwa umoja wetu tuchague njia ya mazungumzo na maelewano kwani itaihakikishia nchi yetu amani, usalama na utulivu. Tukifanya hivyo historia itatuhukumu kwa wema.
↧