Quantcast
Channel: Maisha Times
Viewing all 209 articles
Browse latest View live

Dr. Slaa Apokewa Kifalme Nchini Marekani!

$
0
0

Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani
 
 Dr. Slaa na Mkewe wakilakiwa na Rais wa Chuo  

Moja wa mamea mashuhuri marekani akimsalimia Dr. Slaa


 Dr. Slaa akikaribishwa Ukumbuni kwenye Chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake


Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani



  Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye


  Watoto nao walijitokeza kumsalimia na kupiga picha na mgeni mashuhuri Dr. Slaa


Watu wengi mashuhuri walioalikwa walimiminika kusalimiana na Dr. Slaa



  Dr. Slaa na Senator Shelby wakibadilishana mawazo wakielekea uwanjani



   Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani
 


Watu wa kila aina mashuhuri walifika kumsalimia Dr. Slaa



   Dr. Slaa na Gavana


Dr. Slaa akisalimiwa na mmoja wa US congressmen waliohudhuria mchezo 


   Mshindi wa Nobel Peace Price na Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno


Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri



        Uwanja ulijaa hasa. Watu zaidi ya laki moja walihudhuria



Wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo, Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani

Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa ambayo Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu kama football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na Georgia State. Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama.

Akimkaribisha Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “
Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.

Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football.
Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo.

Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.

Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Dr. Slaa



Kutoka kifungoni Gazeti la Mwananchi laingia mtaani kwa hamasa kubwa!

$
0
0

Nakala ya gazeti la Mwananchi la leo ijumaa tarehe 11.10.2013 ambalo lilikuwa limefunguiwa kwa takribani wiki mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications limited (MCL) Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Denis Msacky. PICHA | FIDELIS FELIX

Akiongeza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuchapisha magazeti ya mwananchi Bw Tido Mhando amesema licha ya kufunguiwa na serikali kwa kipindi cha wiki mbili haitarudi nyuma katika utendaji wake na kuahidi kuendelea kusimamia haki sheria na ukweli daima.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akiwa ameambatana na mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi Bw Denis Msaki ambapo amesema kwa kipindi cha majuma mawili wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 400.

Pinda afuta agizo la Magufuli la wamiliki kutozwa 5% kwa kila gari litakalozidisha uzito!

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. mizengo Pinda (Picha kutoka Maktaba)

 Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. mizengo Pinda

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana amefuta agizo lililotolewa na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli la kuwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo, kutozwa asilimia tano kwa kila gari litakalozidisha uzito na kuagiza kurudiwa kwa utaratibu wa zamani wa msamaha wa asilimia tano ya tozo hiyo.
Pinda pia ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Wizara ya Ujenzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Uchukuzi na Ofisi ya Waziri Mkuu kukutana na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa),Chama cha Wamiliki wa
Malori (Tatoa) ili kukubaliana kwa pamoja kuhusu tozo hiyo. Agizo hilo la Magufuli alilolitoa takribani siku nne zilizopita, liliathiri kasi ya upakuaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam kutokana na mgomo huo wa malori.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Pinda alisema, katika mazingira yaliyopo sasa, ushirikiano kati ya Serikali na wadau unahitajika. “Ni lazima wadau washirikishwe ili kusiwe na malalamiko na mambo yaende vizuri,” alishauri Pinda.
Alisema, awali utaratibu uliokuwa unatumika ulipewa baraka na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu (sasa Ujenzi), Basil Mramba ambaye baada ya wadau wa usafirishaji kulalamika kuhusu ubovu wa barabara na mizani, alitoa unafuu wa kupunguza asilimia tano ya uzito utakaosomwa katika mizani (utakaozidi).
“Lengo lake ilikuwa ni kufidia matatizo ya upungufu wa mizani kutoweza kupima kwa usahihi uzito wa magari yanayopimwa katika vituo mbalimbali vya mizani nchini, lakini hivi sasa mizani yetu ni mizuri na ya kisasa,” alisema na kuongeza:
“Lakini ikumbukwe kuwa agizo hilo lilikuwa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 toleo la 2002 na kanuni zake za mwaka 2001, ambayo inazuia malori kuzidisha uzito. Mramba aliamua vile ili kumaliza hali iliyokuwa imejitokeza wakati akiwa Wizara ya Miundombinu,” aliongeza Pinda. Alisema kati ya kanuni hizo, kanuni ya 7(3) inatoa sharti la kama lori likibainika kuzidisha mzigo,sharti ni ama kupanga upya mzigo ili kupunguza uzito,kuushusha mzigo uliozidi au kupigwa faini mara nne ya faini ya kawaida. Pinda alisema baada ya kuibuka kwa mgomo huo alikutana na wadau wa usafirishaji na mawaziri wa wizara zenye dhamana na ujenzi na usafirishaji, kubaini kuwa kulikuwa na ulazima wa wizara hizo kukutana na wadau ili wakubaliane.
Bandari walia na mgomo
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA),imeeleza kuwa wananchi ndiyo watakaoumia kwa kulazimika kulipa hasara iliyotokana na mgomo huo.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Bandari hiyo, Janeth Ruzangi alisema hali hiyo itatokana na wafanyabiashara kulazimika kupandisha bei ya bidhaa mbalimbali zilizokwama kwa siku kadhaa bandarini hapo ili kufidia gharama walizotozwa na wamiliki wa meli.

Tanzania- Nchi tajiri, Wananchi masikini!

$
0
0

Dhahabu

Tanzanite

Almasi

  Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa kwa watalii

Mbuga na hifadhi mbalimbali za Wanyama ambazo ni kivutio kikubwa kwa watalii.

Wakati taarifa za ukuaji wa uchumi zikionyesha uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia saba kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, bado mamilioni ya Watanzania wanaishi katika lindi la umaskini. Pamoja na ukuaji huu, asilimia 70 ya Watanzania wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ambayo ni sawa na Sh 1,600.
Ni kweli kuwa Tanzania ni tajiri, lakini watu wake ni maskini! Swali hili la kwa nini Watanzania ni masikini linaulizwa na wengi, lakini jibu la uhakika halijapatikana. 
Nchi zinazotajwa leo kuwa tajiri kama Singapore, Korea Kusini, Malaysia na Taiwan zilikuwa pamoja na Tanzania katika fungu la nchi maskini sana duniani wakati tunapata uhuru mwaka 1961.
Nchi nilizozitaja hazina rasilimali nyingi kama Tanzania lakini zimetuacha tukiogelea katika lindi la umaskini wa kutisha licha ya kuwa na madini, gesi na rasilimali za mali asili na ardhi kubwa.
Utajiri wa maliasili ambao Mungu ameijalia Tanzania huwashtua wageni wengi wanaokuja kuitembelea na wengi wanashindwa kuelewa ni kwa nini bado tunaendelea kuwa maskini.
Siku moja nikiwa safarini kuelekea mkoani Arusha kikazi, nilikaa kwenye viti vinavyoambatana kwenye basi nikiwa sambamba na raia mmoja wa China, aliyejitambulisha kwangu kwa jina moja la Xia.
Kipindi chote cha safari tulikuwa hatuzungumzi, japokuwa nilitaka kumdodosa mambo mawili matatu. Nilisita kumuuliza chochote kwa kuhofia tusingeelewana kwenye mawasiliano, nikiamini kuwa lugha anayoijua ni Kichina tu.
Tulipokaribia kufika Wilaya ya Same, alinipa kamera yake na kuniomba nimsaidie kuchukua picha ya safu ya milima ya Upare, ambayo tulikuwa tukiipita kwa sababu nilikuwa nimekaa kiti cha dirishani. Niliifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa, jambo ambalo lilimfurahisha na urafiki ulianzia hapo.
Nilibaini kuwa anaweza kuongea lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa shida baada ya kunishukuru kwa kumpigia picha nzuri. 
Tulianza kuzungumza na katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa amekuwa hapa nchini kwa zaidi ya mwaka na nusu. Lengo lake la kuwa nchini ni kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya madini.
Alisema ameshatembeleza zaidi ya mikoa 15 na wilaya zaidi ya 40 akiangalia fursa za uwekezaji kwenye madini. Kwamba katika nchi za Afrika, mbali na Tanzania, alishatembelea nchi nyingine nane, lakini baada ya kufika Tanzania hakuona sababu ya kuendelea na safari katika nchi nyingine kutokana na fursa za uwekezaji alizoziona.
Mchina huyo alishangaa kwa nini Tanzania ni maskini wakati ina kila kitu cha kuiwezesha kuwa moja ya mataifa tajiri duniani na alinidokezea kwa sauti ya chini kuwa katika tembeatembea yake amekutana na raia wa kigeni wengi wanaojihusisha na biashara ya madini, bila kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
Alieleza kushangazwa na hali ya baadhi ya vijiji vyenye utajiri wa madini, huku wakazi wake wakiishi katika hali ya umaskini mkubwa wakati shughuli za uchimbaji zikifanyika bila usimamizi wowote.
Alichoniambia kwa sauti kubwa ni kwamba usimamizi katika sekta ya madini bado siyo mzuri, jambo ambalo linawapa mwanya wageni kunufaika zaidi.
Siyo jambo la kubishana kuwa ni kweli usimamizi wa uchimbaji madini sehemu nyingi nchini siyo wa kuridhisha, hivyo kampuni nyingi za kigeni zinaneemeka na utajiri wetu kuliko wananchi. 
Serikali imeshindwa kusimamia rasilimali za taifa. Ili tutoke hapa tulipo, viongozi wetu na wananchi tunapaswa kukubali kuwa tumechelewa kuandaa nguvu kazi ya kusimamia na kuendesha sekta za madini na nishati na kibaya zaidi, baadhi ya wanaoteuliwa kusimamia sekta ya madini siyo waaminifu.
Itakumbukwa kuwa, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Mrema, alipata kueleza kuwa alikamata dhahabu ya mabilioni ya shilingi katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam ikisafirishwa kwa magendo kwenda nje ya nchi na mara nyingi tumesikia mchanga wa madini unapelekwa nje ya nchi, huku Watanzania wakiwa hawana la kufanya.
Mara kadhaa pia tumesikia makontena yanakamatwa nje ya nchi yakiwa na nyara za serikali. Ni jambo la kushangaza kuwa nyara hizo husafirishwa ndani ya nchi na kupita hadi zinapovushwa huku kukiwa na ulinzi kwenye mipaka yetu.
Hatujawahi kusikia uchunguzi wa kina uliofanyika na kubaini ni kwa namna gani nyara za serikali zinachukuliwa kutoka porini na kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuupata mtandao mzima na kuuchukulia hatua za kisheria.
Tanzania imeendelea kuwa shamba la bibi ambalo mjanja yeyote anaweza kuja kuvuna na kuondoka pasipo kubughudhiwa. Ni jambo la kusikitisha kuwa katika kazi yangu hii ya uandishi wa habari nimeshashuhudia polisi wakishirikiana na wahalifu kufanikisha vitendo vya kuhujumu rasilimali za nchi.
Makampuni mengi ya kigeni yanaendelea kuonyesha nia ya kuwekeza kwenye gesi pamoja na uranium. Lakini yote yanataka kupewa mazingira mazuri ya uwekezaji (favourable investment condition) ili yaweze kuleta mitaji yao hapa nchini. 
Yapo malalamiko kuwa makampuni makubwa ni vinara wa kukwepa kodi, lakini serikali imeshindwa kuyashughulikia. Watu wa kawaida wenye vipato vidogo na vya kati, wakiwamo wafanyakazi ndio wanaolipa kodi kwa kuwa imeambatanishwa kwenye bidhaa wanazonunua na kwenye makato ya mishahara yao.
Ukwepaji kodi nchini hufanywa na makampuni makubwa kwa njia mbalimbali, ikiwamo kudanganya thamani ya mali zao, bidhaa na faida wanazopata ili mamlaka husika ziyatoze kodi ndogo.
Inakadiriwa kuwa, udanganyifu unaofanywa na makampuni ya madini unaifanya nchi ipoteze mapato yanayofikia dola za Kimarekani milioni moja kwa mwaka, sawa na Sh 1.6 trilioni ambayo ni sawa na bajeti ya miaka mitano ya Wizara ya Kilimo, ambayo ni Sh bilioni 200 kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Hii ndiyo Tanzania niliyoitazama leo, nchi tajiri, lakini watu wake maskini.

Mtangazaji wa itv apigwa risasi, mama yake auwawa na mume wake kujiua!

$
0
0
Pichani ni mtangazaji wa kituo cha Television cha ITV Ufo Saro katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na waandishi mbalimbali Ikulu Decemba 12, 2012 (Picha kutoka Maktaba)

Kuna taarifa kwamba mtangazaji wa kituo cha Television cha ITV (Ufo Saro) amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya huko maeneo ya Kibamba leo Alfajiri na mama yake mzazi kuuliwa. habari zaidi zinasema kwamba aliyefyatua Risasi hizo ni mchumba wa Mtangazaji huyo anayefanya kazi katika shirika moja la UN, ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua. 

Maisha Times Blog inaendelea kufuatilia tukio hili la kuhuzunisha na punde itakuletea habari hii kwa kina. Endelea kuwa nasi.

Source: Breaking News - Radio One


Ripoti kamili ya mauwaji ya kinyama Mauaji ya kutisha

• MTANGAZAJI ITV APIGWA RISASI NA MCHUMBA WAKE

MTANGAZAJI wa kituo cha runinga cha ITV, Ufoo Saro amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi mbili tumboni na kifuani na mzazi mwenzake, Antel Mushi ambaye ni mhandisi wa mawasiliano kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa (UN) kinachofanya kazi nchini Sudan.

Katika tukio hilo la kutisha lililotokea jana saa 12:30 asubuhi, Mushi pia alimuua mama mzazi wa Ufoo kwa kumpiga risasi kifuani na kisha kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi eneo la kidevu, iliyomfumua kichwani.

Mauaji hayo yalitokea eneo la Kibamba, Njia panda ya Shule, nyumbani kwa mama mzazi wa mtangazaji huyo, Anastazia Salo (58) ambako wawili hao; Ufoo na mpenzi wake walikuwa wamefika muda mfupi kabla tukio.

Mushi na Ufoo wamezaa mtoto mmoja, Alvinen Mushi (10), na wakati wanatoka nyumbani kuelekea kwa mama mzazi wa mtangazaji huyo, walimuacha mtoto wao akiwa amelala na dada yake wa kazi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, tukio hilo linahusishwa na ugomvi wa kifamilia ambao hadi sasa haujafahamika chanzo chake.

Shuhuda wa tukio hilo, Habelis Innocent ambaye ni ndugu wa karibu wa Ufoo, aliliambia gazeti hili kuwa mtangazaji huyo alijeruhiwa vibaya eneo la tumboni na mkononi.

Habelis alisema kuwa mapema alfajiri jana, Ufoo na Mushi waliondoka nyumbani kwao eneo la Magari Saba kuelekea Kibamba kwa mama wa Ufoo, kwamba wakiwa njiani mtangazaji huyo alimpigia mama yake simu na kumwambia aondoke nyumbani haraka.

Alisema kuwa Ufoo alimtaka mama yake kuondoka nyumbani kwa kuwa mchumba wake ana hasira, na hivyo anaweza kufanya fujo, lakini baada ya mama huyo kupata taarifa hizo hakuweza kuondoka haraka hadi walipofika.

Habelis alifafanua kuwa walipofika nyumbani hapo waligonga mlango na kisha mama yao kuwafungulia. Kwamba muda huo alikuwa anajiandaa kwenda kanisani, lakini hakuweza tena kuendelea na alichokua anakifanya, badala yake aliketi kuwasikiliza kilichowaleta.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, wakati mama, Ufoo na Mushi wakiwa sebuleni yeye alikuwa chumbani huku akisikia mazungumzo yaliyodhihirisha kulikuwa na mgongano ambao ulitakiwa kutafutiwa ufumbuzi.

Alisema kuwa wakati mazungumzo hayo yakiendelea, ghafla akasikia mlio wa risasi na sauti ya mama akiomba msaada kutoka kwake, akimtaka atoke haraka aliko ili kama kufa wafe wote.

Habelis alisema kuwa alipotoka alikuta tayari mama yake ameuawa na baadaye Mushi alimpiga risasi ya tumboni na mkononi Ufoo.

“Baada ya kushuhudia tukio hilo, nilianza kujihami na kukimbilia kwenye chumba kingine huku nikiwaambia wenzangu niliokuwa nimelala nao wasitoke nje.

“Wakati natafuta namna ya kujihami kwa kupanda darini, Mushi alipiga risasi nne mfululizo ili mlango ufunguke zinipate, lakini alishindwa na hivyo alihamia chumba alichokuwa mdogo wa Ufoo na kupiga risasi mbili mfululizo ili zimpate yoyote aliyekuwemo,” alisema.

Aliongeza kuwa wakati akipiga risasi hizo, vijana waliokuwa katika chumba hicho walifanya jitihada za kubomoa dari na kisha kupata upenyo wa kujificha darini na hatimaye Mushi akawakosa.

Aliwataja wenzake hao waliokoswakoswa na risasi katika tukio hilo kuwa ni Godluck Saro na Jonasi Saro na kuongeza kuwa baadaye Mushi alikimbilia jikoni na kukuta jiko la gesi, aliwasha na kuchoma nguo ili nyumba ilipuke waliomo ndani wateketee.

Shuhuda huyo alisema kuwa baada ya kuchoma nguo, Mushi alirudi sebuleni na kisha kujimalizia mwenyewe kwa kujipiga risasi na kupoteza maisha papo hapo.

Ufoo alikimbizwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha ambako alipatiwa huduma ya kwanza na kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, uchunguzi wa awali uliofanyika katika gari alilotumia Mushi walikuta begi likiwa na kompyuta ndogo (laptop), kamba za kujinyongea, panga, pingu, kisu na risasi.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini Muhimbili, Kova alisema kwa mujibu wa madaktari, hali ya mgonjwa ilikuwa inaendelea vizuri na alikuwa akitarajiwa kufanyiwa upasuaji nyakati za mchana.

Kova alisema japo mhusika alijiua baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi kwa risasi Ufoo, bado kitendo hicho hakiliondolei jeshi hilo kuchunguza tukio hilo.

Alisema kuwa wanatarajia Ufoo atakuwa miongoni mwa watu watakaolisaidia jeshi hilo kupata taarifa zaidi za tukio hilo.

Naye, ofisa upelelezi wa makosa ya jinai, Ahmed Msangi alisema hadi sasa hakuna taarifa kamili, bali jeshi limejigawa sehemu tatu, kila kundi likikusanya taarifa.

Alisema baada ya makundi hayo ambayo yalikuwa katika maeneo ya nyumbani lilikotokea tukio, Tumbi hospitali na Muhimbili, kukusanya taarifa watazitoa kwa waandishi wa habari.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi alisema kipindi hicho madaktari walikuwa wakiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kukamilisha upasuaji.

Alisema kuwa hali yake Ufoo sio mbaya bali ilikuwa inaendelea vizuri akiwa chini ya uangalizi wa madaktari

Miaka14 ya kummkumbuka baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere! Haya ni mambo11 aliyoyapinga.

$
0
0
Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere [1922-1999]

HAYA NI MAMBO (11) YALIYOYAPINGWA NA BABA WA TAIFA

Ni miaka kumi na nne sasa imepita tangu mzee wetu mpendwa baba wa taifa hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aiage dunia.
 
Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 13, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria . Alikuwa ni mototo wa chifu Burito Nyerere wa kabila dogo la wazanaki
Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani. Mwalimu bado ni taa inayong’aa gizani, umuhimu wake nazidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda licha ya kwanza amekwisha tuacha.
Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:

1. UJINGA
 

Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache na ni mtanzania wa kwanza kupata nafasi yamasomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburg , Uingereza na kuhitimu mwaka 1952 akiwa ni gwiji wa uchumi na historia.
 
Mwalimu hakupenda ujinga na hivyo alipigana vita kali dhidi ya ujinga, na alifanikiwa kwa nafasi yake kuwaondoa ujinga watanzania wengi, wakiwemo viongozi wetu wa sasa ambao walisomeshwa ‘bure’ katika mazingira mazuri yakuridhisha kwa manufaa ya nchi yetu. Ndiyo maana Rais Kikwete Februari 3, 2007 alisema “….sisi tuliwekezwa na ni lazima tuwekeze kwenu ili miaka 30 ijayo Rais atoke miongoni mwenu….”
Kama Nyerere asingechukia ujinga kwa kuboresha mazingira ya elimu, ikiwemo elimu ya watu wazima, basi leo hii tungekuwa na vingozi ‘zezeta’.
Vita ya ujinga sasa si yakuridhisha. Zaidi ya asilimia
28.6 ya watanzania hasa waishio vijijini hawajui kusoma na kuandika, pamoja na kutoa elimu ya msingi bure na kupunguzwa ada ya sekondari na kuongeza idadi ya madarasa, bado shule hizi zinakosa waalimu na vifaa vya kutosha. Pia idadi kubwa ya watanzania pamoja na kufaulu hawapati nafasi ya elimu ya juu kutokana na sera chakavu na mifumo kndamizi iliyopo nchini, kama ya kuangalia madaraja [Division] katika utoaji wa mikopo na asilimia za uchangiaji gharama za elimu ya juu.
Kuna usemi usemao “If education is Expensive try ignorance as your option” [kama elimu ni ghali, jaribu ujinga]. Serikali yetu ni wazi kabisa kuwa inaona elimu ni gharama, hivyo imeamua kujaribu ‘ujinga’ kwa kile inachokiita ‘kuchangia elimu ya juu’ eti serikali haina uwezo.
Huku ndiko kuzienzi kuzienzi fikra za Mwalimu Nyerere?

2. UBINAFSI NA UFISADI 


Katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo wa aina yake, ni pamoja na masuala ya haki na usawa. Mwalimu siku zote, alijenga imani katika misngi ya utu, haki na usawa kwa kila raia wa dunia hii. Aidha Mwalimu alipinga sana mianya ya unyonyaji aliyoiita ‘mirija’. Mwalimu alipinga sera zozote zinazweza kuleta matabaka katika Taifa, iwe ni matabaka ya kiuchumi kwa kuwa na kundi la walionacho na wasionacho. Mwalimu hakuruhusu ubinafsi na ufisadi ambao ambao leo hii umekithiri miongoni mwa viongozi wengi hapa nchini. Mwalimu aliwahi kusema “Hakuna mtu yeyote katika jamii atakayekuwa na mahitaji yote muhimu wakati wengine katika jamii hiyohiyo hawana chochote”. 
Mwalimu alijikita katika siasa ya ‘ujamaa’ na kujitegemea na hatimaye Azimio la Arusha mwaka 1967, ili kahakisha keti ya Taifa [National cake] inakuwa na mgawanyo sawa kwa wote.Leo hii Azimio la Arusha limesahauika kabisa, hali ya viongozi wa serikali wanatanguza mbele maslahi binafsi hali ambayo baba wa Taifa aliipinga tabia hiyo chafu inayozidi kuchukua sura mpya kila kukicha.
Mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa katika wakati mgumu wa vita dhidi ya Nduli Iddiamin Dada, lakini wabunge walihitaji nyongeza ya mishahara na kupunguzwa posho ya waanafunzi wa elimu ya juu. Hali hii ilipelekea wanafunzi wa enzi hiyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kugoma na kupinga ubinafsi wa waung hao. Hapa tuliona msimamo, uzalendo na busara za Mwalimu aliyetoa kauli kali ya kuamuru mishahara ya wabunge ipunguzwe na posho za vijana zibaki kama awali.
Nyerere asingekuwa mzalendo wa kwelil basi leo hii familia yake wangekuwa ndio mabilionea wan chi hii.

3. UBEPARI
 

Mwalimu alikuwa ni nuru ing’aayo gizani, alipinga mfumo wa ubepari kwa kuuita ‘mfumo wa ufukarishaji’. Hivyo aliimarisha misingi imara katika itikadi yake ya ujamaa na kujitegemea, ikiwa ndiyo itikadi pekee yenye misingi ya utu, haki na usawa.
 
Mwalimu alichukizwa sana na mfumo mpya wa kibepari uliozuka baada ya yeye kung’atuka madarakani aliouita ‘ubepari wa pembezoni’ yaani ni ubepari wa kishenzi unaotoa mianya kwa wachache kutumia mirija kuwanyonya wanyonge. Tanzania yetu leo hii, bila hata aibu katiba ya Jamhuri ya Muungano katika ibara yake ya 3 inasema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Hili linaleta utata na mkangnyiko kwani kimaandishi ni wajamaa lakini matendo yaliyopo ni zaidi ya ubepari.
Unaweza kuangalia uuzwaji holela wa nyumba za serikali zilizojengwa kwa jasho la Mzee Nyerere na akina Rashid Kawawa, pamoja na mikataba mibovu inayotanguliza maslahi ya wachache.Mwalimu hakusita kukemea mambo ya kihuni kama haya. Katika kitabu chake Ungozi wetu na hatima ya Tanzania ukurasa wa 28 Mwalimu alisema “Halimashauri kuu ya Taifa iliketi unguja, ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi, na walikuwa na haki ya kufanya hivyo maana sera ni yao.Ubaya wao ni kwamba, jambo lenyewe walilifanya kwa hila na janjajanja na mpaka sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM ni ya ujamaa na Kujitegemea.”

4. UKABILA NA USEHEMU
 
Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam , alifanikiwa kuwaunganisha wanafunzi katika jumuiya moja iitwayo USARF ikijumuisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika. Aliona kuwa ni vema kwani Afrrika ni moja. Leo hii wanafunzi wetu wanajitambulisha na kujitanabaisha kwa makabila na sehemu watokazo. USARF imekufa kabisa na imebezwa na vijikundi vya makabila yao . Hali hii ya ukabila na usehemu inatawala kona zote za nchi yetu na ndiyo maana watu wengi wakienda kuomba kazi au hata huduma katika sehemu fulani, utasikia anaulizwa ‘wewe ni kabila gani au unatoka mkoa gani?’Hapa tulipofikia nchi yetu imepotea kisiasa, kijamii na hata kiuchumi.
Naamini Roho ya Mwalimu Nyerere inahuzuika sana kuona wanafunzi wanavyomkumbuka wakidai haki zao hasa katika vipindi vya migomo, wakati hili ambalo aliasisi hawalienzi.

5. UBINAFSISHAJI HOLELA WA MALI ZA UMMA
 

Wakati wa uhai wake Mwalimu alilaani vikali ubinafsishaji holela wa masirika ya umma. Alwakataa Mabeberu waliojiita ‘wawekezaji’ walionuiya kufirisi utajiri wan chi yetu huku wakishibisha matumbo yao .
 
Leo hii vigogo wa serikali wanajichukulia majumba ya serikali bila kujali wao kutoka madarakani watumishi wa umma hapo baadaye wataishi wapi.
Huku ndiko kumuenzi Mwalimu, aliyekataa kuishi kwenye nyumba kubwa kule Butihama, akisema yeye sio tembo? Uko wapi uzalendo aliotuachia Mzee Nyerere?

6. KUONGOZWA KWA RIMOTI NA NCHI MATAJIRI
 

Nakumbuka siku moja Mwalimu Nyerere akiwa katika viwanja vya mnazi mmoja [Dar es salaam] aliwahi kusema “Tangu lini IMF ikawa International Ministry of Finance?” [Wizara ya fedha ya kimataifa].
 
Leo hii viwanja hivyohivyo vinatumika kuusifu ubeberu wa IMF na wawekezaji wake, huku tukiwekewa masharti magumu ya kuongoza nchi yetu kwa maslahi ya mabeberu.
Mwalimu aliwaonya mataifa tajiri wasiingilie mambo yetu ya ndani, pale walipoona maslahi yao hayazingatiwi, mara kwa mara walimuhoji Mwalimu ambapo yeye aliwaamuru waondoke haraka na misaada yao yote. Mwalimu hakupenda misaada ya kinafiki iliyolenga kuwaangamiza wananchi wake, alipinga amri na maagizo ya taasisi za fedha kama Benki ya Dunia [WB] na IMF [International Monetary Fund].Hivyo aliheshimu maamuzi yake sahihi katika kulinda heshima ya nchi yetu na watu wake.
Kipindi chote cha uhai wake Mwalimu alisisitiza haja ya mataifa ya Afrika kujitawala na kuwa huru katika kujiamulia mambo yake. “Inapotokea taifa kuuza uhuru wake kwa ajili ya misaada ya kiuchumi au kukubali kukaliwa na majeshi ya nje, taifa hilo linakuwa limepotea na litanyonywa na watu wake watakuwa wanakandimizwa popote pale” alisema Mwalimu.
Kama tungekuwa na misimamo kama Nyerere, tungeheshimika. Lakini leo hii Mwalimu angefufuka angefadhaika sana kuona jinsi tunavyomuenzi.

7. UBABE NA VITISHO KATIKA UONGOZI


Mwalimu aliamini kuwa kiongozi bora hapaswi kuwa na jazba na asiyetumia ubabe wala vitisho katika maamuzi au katika kutatua tatizo ambalo jamii inataka litatuliwe kwa maslahi na manufaa ya Taifa. Aliamini kuwa kiongozi bora ni yule anayeruhusu mianya ya majadiliano baina yake na wale anaowaongoza. Asiyetumia lugha chafu au kashfa na kejeli kwa watu wake.
Leo hii tawala mbalimbali zikiwemo taasisi za elimu ya juu na hata chombo cha juu kabisa cha maamuzi [Bunge] vinatumia ubabe na vitisho katika maamuzi.
Tunashuhudia migomo ya vyuo vikuu kila kukicha huku maamuzi ya ‘kibabe’ yakitumika na watawala wa vyuo katika kukandamiza haki za wanafunzi. Masikini wanafunzi hawa wanabaki wanalia huku wakiimba “… kama siyo juhudi zako Nyerere na ...angesoma wapi…”
Tunaona pia Bunge linavyopitisha maamuzi yasiyo na maslahi kwa wananchi ‘kibabe’ na hata kuadhibu wale wanaojaribu kutetea maslahi ya wanyonge. Bunge hilohilo linatumia pia lugha za kejeli na dharau kuwatisha wananchi, ubabe na vitisho si misingi ya demokrasia na utawala bora.

8. UMANGIMEZA NA UKIRITIMBA

 
Wakati wa uhai wake Mwalimu aliheshimu mipaka, taasisi za utawala na mali za umma. Alichukia matumizi mabaya ya rasilimali za umma, pia aliheshimu mawazo yake mwenyewe na ya wenzake.
Mwalimu aliamini kwamba, kiongozi asiyepeda ukiritimba na umangimeza ni lazima awe mfuasi mzuri wa maadili anayoyasimamia, mwaminifu na mwadilifu kwa manufaa ya Taifa lake. Mwalimu hakupenda kutetea uovu wa viogozi eti kwa kutunza heshima zao au kulinda vyama vyao bila kujali uhusiano wao wala majina yao . Hivyo katika serikali yake Mwalimu hakuawa na ubia na mtu yeyote duniani.
Leo hii ni viongozi wangapi wanadumisha fikra na misimamo ya Mwalimu kwa vitendo?

9. USIRI WA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA KIGENI
 

Mwalimu alisisitiza uwazi katika mikataba mbalimbali ambayo serikali iliingia na makampuni ya kigeni.
Katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo Mwalimu anasema “Viongozi wa kiserikali wana wajibu mkubwa wa kuwafahamisha wananchi nini serikali inafanya na kwa sababu gain”
Tofauti kabisa hali ilivyo sasa, hali inayopelekea minung’uniko na malumbano yanayo husisha hata ugawaji wa tenda za serikali. Labda tuangalie mfano mmoja tu wa Mkataba wa Buzwagi ambao ulikuwa ni maarufu kama ‘Mkataba wa Karamagi’ kati ya Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Kampuni ya Barrik Gold Mine. Mkataba huu ulikuwa ni siri kubwa baina ya Barrik na Waziri tu, hali iliyopelekea Mbunge Zitto Kabwe kusimamishwa shughuli za bunge kwa miezi minne baada ya yeye kuhoji uhalali na uharaka wa utiaji saini mkataba huo uliosainiwa hotelini [Churchil Hotel] mjini London Uingereza.
Hivi nchi yetu itakuwa kituko mpaka lini? Mbona hatuoni viongozi wanaoleta tija na maendeleo.
Nakumbuka Rais Thabo Mbeki wa Afika Kusini alitudharau sana alipokuwa katika moja ya ziara zake hapa nchini, alisema wakati biashara ya Tanzanite inatoa dola milioni 500 kwa mwaka duniani, Tanzania nchi pekee duniani yenye madini hayo inapata dola 80 tu. Rais Mbeki alitukejeli kwa kusema hakuna sababu ya kumtafutamchawi wakati sheria ya uchimbaji madini tumeitunga wenyewe inayoruhusu wageni waondoke na asilimia kubwa ya madini hayo na sisi kuambulia mashimo.
Hali hii inanipa shaka hasa nikichunguza upeo wa kufikiri wa hawa viongozi wetu, ndipo ninapokumbuka usemi wa Waziri mstaafu Arcado Mtagazwa [CCM] alioutoa bungeni mwaka 1993, alisema “Tutakapokufa vizazi vijavyo vitafukua makaburi yetu ili vione vichwa vyetu viongozi vilikuwa na ubongo wa aina gain kwa sababu yaelekea hatufikiri sawasawa”.
Kauli hii ililazimika kutolewa baada ya kuona kwamba baadhi ya maamuzi yanayofikiwa na serikali yetu hayana maslahi kwa taifa na ni ubinafsi.

10. RUSHWA
 

Katiba ya CCM katika ahadi yake ya nne [4] ina sema “rushwa ni adui wa haki, sitatoa rushwa wala kupokea rushwa”. Jambo la rushwa pia Mzee wetu mpendwa Mwl Nyerere alilikemea vikali enzi za uhai wake kwani alijua wazi kuwa rushwa ni kikwazo cha maendeleo ya umma katika kila Taifa.
Leo hi inchi yetu imegubikwa na rushwa na hata kuhalalishwa na kuitwa ‘takrima’ ili tu kukidhi matakwa na mahitaji ya ‘mahafidhina’. Viongozi wa serikali, viongozi katika taasisi mbalimbali wameweka mbele rushwa kama msingi wa kushibisha matumbo yao. Baya zaidi hata viongozi wa CCM chama pekee kilicho asisiwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere wamezisahau kabisa falsafa zake na chuki yake dhidi ya rushwa na hata katika Chaguzi mbalimbali za Chama Cha mapinduzi zilizofanyika siku chache zilizopita tumeweza kusikia kama sio kushuhudia vitendo vya rushwa vikifanyika waziwazi katika chaguzi hizo jambo ambalo licha ya kushindwa kutumia mamlaka aliyonayo katika kuviasaidia vyombo husika kuchukua hatua za kisheria amebaki akilalamika na kushtaki kwa wananchi kuhusiana na vitendo hivyo vichafu vinavyotendeka ndani ya CCM, Serikali na hata katika sekta nyinginezo nyingi nchini. Nakumbuka Mh Kabuye [Mb-TLP] aliwahi kuwashutumu bungeni kuwa anauhakika wabunge wote waliingia kwa rushwa, wabunge hao walioshutumiwa walimtaka Kabuye afute kauli naye alisema “ kwa kulazimishwa nafuta kauli”. Walimlazimisha lakini hoja yake ilibaki kuwa ni ya msingi.

11. UCHU WA MADARAKA
 

Mwl Nyerere ni miongoni mwa viongozi wachache sana duniani waliokosa kuwa na uchu wa madaraka. Ni miaka 24 sasa tangu Mwl ang’atuke madarakani kwa hiari yake akiwa kama rais wa awamu ya kwanza wa nchi yetu na ni miaka 22 tangu aachie uongozi wa CCM kama Mwenyekiti wa chama. Ndipo alipoamua kwa hiari yake kurejea Butihama na kuendeleza kilimo.
 
Uroho wa madaraka leo hii umekithiri, viongozi wengi wanaendelea kung’ang’ania madaraka bila kujali uzee walionao. Mahafidhina hawa wamezoea kusema ‘vijana ni taifa la kesho’ ili wao wazee waendelee kuhujumu mali za nchi yetu. Na unafiki wao ni pale wanaposema ‘vijana ni nguvu kazi ya taifa’, sentensi hizi mbili kimantiki zinakinzana. Mbaya zaidi na kinachouma ni pale unapoona watoto wa vigogo au viongozi wa Serikali wakiwa ndio kama warithi wa nafasi za wazazi wao ndani ya CCM na hata Serikali ya CCM. Hili linaweza kujithibitisha wazi iwapo utaamua kufuatilia kwa undani idadi ya watoto wa vigogo na Viongozi waliomo ndani ya CCM sambamba na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi [CCM]
 

SAKATA LA RUZUKU; CHADEMA wamwaga Nyaraka za 'Siri', Msajili, CAG wawajibike‏!

$
0
0





C/HQ/ADM/KUH/18                                                   17/10/2013

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU MWAKA 2009-2013.

Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.

CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;
     i.         Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.NaCDA.112/123/01a/37, ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa).
Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, tuliziwasilisha kwa Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe 27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa)
    ii. Kuhusu taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye ofisi za msajili wa vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya Novemba 26, 2012 yenye Kumb.Na.DA.112/123/16A/97 ambayo ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).
    iii. Kuhusu taarifa ya fedha kutoka nje ya nchi, CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata fedha kwa ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama ambavyo msajili alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni taarifa ya mapato yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa barua husika )
   iv.Kuhusu Taarifa za gharama za uchaguzi kwa mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni vyama viwili tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa ukaguzi wa marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16 April, 2012. (Nakala imeambatanishwa)
     
     Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya siasa.

Aidha, kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG akague fedha zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge inataka iwe.

Imetolewa leo Alhamis, Oktoba 17, 2013;
……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la Wadhamini. 


SAKATA LA RUZUKU; Baada ya CHADEMA sasa CUF nao wajisafisha!

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF – Tanzania Bara Julius Mtatiro.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - 20/10/2013.
CUF HAIHUSIKI KATIKA HOJA YA VYAMA KUTOWASILISHA HESABU ZAKE OFISI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI.
Chama Cha Wananchi CUF kinapenda kuwajulisha watanzania kwa ujumla kuwa, kimetekeleza sheria mbalimbali ambazo zinataka vyama vya siasa vipeleke hesabu zake ili zikaguliwe na vyombo maalum vya serikali.
Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 14, vyama vilivyo na usajili wa kudumu vinatakiwa kuwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa hesabu za kila mwaka zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali(CAG). Sheria hii ina maana kuwa kwa CAG vyama vinapita kama PROCESS na kwamba kwa MSAJILI ndipo hasa vyama vinapaswa kupeleka ripoti ya hesabu zilizokaguliwa na CAG.
Hiyo ina maana kuwa vyama sasa vinawasilisha hesabu zisizokaguliwa kwa CAG na CAG ambaye ni ofisi ya serikali ana jukumu la kufanya ukaguzi mpana zaidi mpaka ajiridhishe na hiki ndicho CUF imekuwa ikitekeleza.
Hesabu za mwisho ambazo CUF imeziwasilisha kwa MKAGUZI MKUU WA SERIKALI ni zinazoishia tarehe 31/12/2011 ambapo ziliwasilishwa tarehe 11/09/2012 kupitia barua yenye kumbukumbu namba CUF/AK/DSM/KM/OO3/1A/2012/39 iliyosainiwa na MKURUGENZI WA FEDHA WA CUF ndugu. Salim Mandari iliyokuwa na kichwa cha habari “KUWASILISHA HESABU ZISIZOKAGULIWA KWAKO KWA AJILI YA UKAGUZI HESABU ZINAZOISHIA 31/12/2011”.
Hatua hii ilitokana na kutekeleza sheria pamoja na maelekezo ya barua ya msajili wa vyama vya siasa iliyokuwa na kumbukumbu namba CDA.112/123/01A/37 ambayo ilimtaka Katibu Mkuu wa chama chetu awasilishe hesabu zisizokaguliwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali kama hatua ya MSAJILI kukimbusha chama.
Tumesikitishwa na kauli tulizozisikia kupitia katika vyombo vya habari kuwa chama chetu ni miongoni mwa vyama kadhaa ambavyo havijawasilisha hesabu kwa mkaguzi mkuu wa serikali kwa kipindi cha miaka minne sasa. Tunaomba watanzania wazipuuze taarifa hizo kutuhusu kwa sababu hazina ukweli wowote.
Chama Cha Wananchi CUF pia kinapenda kuujulisha umma kuwa hesabu zake ambazo hazijawasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ni zile zinazoishia tarehe 31/12/2012 ambazo wakaguzi wa ndani na wa nje wamemaliza kuzikagua mwezi Julai mwaka 2013 na zitathibitishwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa cha mwezi Oktoba 2013 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokaa mwezi Novemba 2013 na kisha zitawasilisha kwa CAG kabla ya mwezi Desemba 2013. Hii ina maana kuwa hesabu ambazo hazijamfikia msajili ni za mwaka mmoja uliopita na siyo miaka minne kama ambavyo kamati ya PAC imetangaza.
Chama chetu kimesikitishwa na kufadhaishwa na hatua ya kamati kuvihukumu vyama vyote vya siasa wakati jambo hili ni la chama kimoja kimoja. Na mbaya zaidi ni pale ambapo mwenyekiti wa kamati ya PAC mhe. Zitto Kabwe amekuwa akishinda kwenye mitandao ya kijamii “akishupalia” kuvichukulia hatua vyama – kikiwemo chama chetu huku hana taarifa za kina za namna tulivyotekeleza wajibu wetu.
Ikiwa kamati ya bunge inashinda kwenye mitandao ya kijamii ikihukumu na kutoa taarifa za uongo kwa umma bila hata kuwasiliana na vyama vya siasa ni jambo la kufedhehesha mno. Kamati makini ya bunge ni ile ambayo inapokea taarifa kutoka pande zote muhimu, inakutana na wadau wote na kisha inajua tatizo liko wapi na kuujulisha umma nani amesababisha uzembe.
Kwa sababu kamati hii imeligeuza jambo hili kuwa mtaji wa kisiasa na kukitangaza chama chetu kuwa hakikutambua wajibu wake jambo ambalo siyo sahihi, Chama chetu kinatafakari hatua za kuchukua ikiwemo kumuandikia Spika ili azifundishe kamati zake namna bora ya kufanya kazi zake kama kamati za umma.
Chama chetu pia hadi leo hakijapokea barua yoyote ya kuitwa na kamati ya bunge ya hesabu za serikali siku ya tarehe 25 Oktoba. Kwa hiyo, CUF haitahudhuria katika kikao hicho kwa habari za kuitiwa kupitia kwenye FACEBOOK, TWITTER, WHATS UP n.k.
Kama kamati inatuhitaji twende kuifafanulia taarifa za upande wa pili baada ya kumaliza kazi yake ya kutuchafua, na ituandikie barua rasmi ya kutuita tarehe 25, tukipata barua tutakwenda. Ikiwa hatuitwi tarehe hiyo kwa barua rasmi hatutakwenda na kamati ya PAC haitakuwa na "LOCUS STAND" ya kutuhoji mahali popote pale.
Tunapenda watanzania waelewe kuwa chama chetu kimekuwa pekee ambacho kimepata hati safi za ukaguzi wa fedha kila mara tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na hatukuwahi kupata doa wala kashfa katika masuala ya fedha.
Mungu Ibariki Tanzania!
“HAKI SAWA KWA WOTE”
Julius Mtatiro, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wananchi CUF – Tanzania Bara.

Huyu ndiye Mtanzania anayetudhalilisha watanzania nchini Uingereza!

$
0
0
 Flora Lyimo akiwa kazini

 Kushoto ni mwanadada Flora Lyimo akiwa katika picha ya pamoja na Naibu katibu Mkuu wa CCM Taifa Mhe. Mwigulu Nchemba wakati alipofanya ziara yake nchini uingereza.

Flora Lyimo katika moja ya pozi zake

Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa haswa kwa baadhi watanzania wanaoishi nje ya nchi haswa haswa wale wanaoishi katika nchi mbalimbali za ulaya kufanya vitendo visivyo vya kistaarabu na vinavyolenga moja kwa moja kuudhalilisha sio tu utu wa mwanadamu bali kumdhalilisha Mtanzania na Taifa zima kwa ujumla wake. 


Swali langu ni je Sheria za nchi yetu zinasemaje kuhusiana na watu wa aina hii, Kama hakuna sheria inayoweza kusimamia tabia kama hii je Serikali ina mpango gani? Au serikali na wananchi kwa ujumla tumeridhika? 



INASIKITISHA: Julius Nyaisanga alisalitiwa na wenzake!

$
0
0
Marehemu Julius Nyaisanga

Sio vyema kukumbushia habari zao waliolala mauti. Waacheni wafu wazike wafu wao, ndivyo maandiko yanavyosema. Lakini katika hili la Nyaisanga tuna la kujifunza hasa kwa sisi wenye taaluma ya habari..

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya familia zinadai kuwa wakati Nyaisanga alipokuwa mgonjwa, hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afy
a yake.

Alisumbuliwa na kisukari kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna aliyejali. Si waajiri wake (ambao Nyaisanga aliwaingizia mamilioni ya fedha kwa umahiri wake wa kazi), si wanahabari wenzie, wala marafiki zake.

Licha ya kusumbuliwa na maradhi muda mrefu na licha ya wenzie kutoonesha support lakini, hakujali, aliendelea na kazi zake.

Wakati Radio One inaanzishwa alikubali kujitoa sadaka na kuacha kazi RTD ili kuhakikisha Radio One inaanzishwa na inasimama imara. Wakati ule na kina Charless Hilary, Mickdady Mahmood, Flora Nducha, Abdalah Majura na wengine.

Mtangazaji mararufu wa BBC, Aboubakar Liongo anadai ni Julius aliyemshawishi kuingia kwenye taaluma ya habari. Ni yeye aliyempeleka Radio One kufanya majaribio yake ya kwanza kama Radio Presenter. Hata baba yake Liongo alipoonesha wasiwasi Nyaisanga ndiye aliyemtoa wasiwasi huo kwa kumhakikishia usalama wa mwanae.

Hata baadae iliporipotiwa amesimamishwa kazi Radio One licha ya kuitumikia kwa takribani miaka 15, hakukata tamaa, aliendelea kupambana. Hatimaye akapata ajira Abood Media Morogoro.

Alipokuwa Morogoro bado aliendelea kusumbuliwa sana na kisukari na pressure. Aliugua, alizidiwa, akalazwa, lakini hakuna aliyekuwa karibu yake zaidi ya familia yake. Si watangazaji wenzie maarufu aliokuwa nao enzi hizo, au waajiri wake aliowatumikia kwa uaminifu.

Hata aliporipotiwa kuzidiwa na kwamba hali yake ilikuwa "serious" hakuna aliyejali. Alihangaika na mkewe na wanae huku akipewa support "kidogo" na Mzee Abood.

Licha kuzidiwa na maradhi lakini alilazwa "zahanati" ya Mazimbu, inayodaiwa kuwa Hospitali. Na bila shaka kutokana na kutopata huduma alizostahili kwa maradhi yake akafariki dunia.

Lakini mi nadhani Nyaisanga alihitaji matibabu bora zaidi ya yale ya Mazimbu. Alihitaji hospitali kubwa zaidi ya ile dispensary inayodaiwa kuwa hospitali pale Mazimbu. Pengine asingefariki ikiwa angepata huduma "standard" kidogo kwenye hospitali ya kueleweka.

Haikuwa lazima apelekwe Muhimbimbi kwenye VIP wodi, kama aliyopo Ufoo Saro. Nyaisanga hakuhitaji wodi yenye TV set, flat screen kama aliyopo Ufoo.. Alihitaji wodi ya kawaida yenye madaktari wataalamu ambao wangeweza kutatua shida yake.

Lakini ndio hivyo uwezo wake haukuruhusu kufika huko. Akaishia Mazimbu. Akaugua, akateseka, akalazwa. Peke yake. Hata wandishi wenzake hawakuandika habari za mwenzao kuugua.

However hata hawakumtembelea japo tu kumjulia hali hata kama walikuwa hawataki kuandika. Nani angemtembelea na wote walikuwa busy na risasi za Ufoo Saro..???

Aliugua, akateseka, akapita katika bonde la uvuli wa mauti. Licha ya kuwa alikuwa peke yake lakini hakuogopa, maaana "gongo na filmbo" yake BWANA vilimfariji.

Hatimaye akafariki usiku wa kuamkia October 20. Na hapo hasa ndipo ulipoonekana USALITI na Unafiki. Kila mtu alijifanya kumfahamu. Kila mtu alijifanya rafiki yake. Hata wale rafiki zake ambao pengine tangu waachane Radio One hawakuwahi hata kumpigia simu wakajifanya kuomboleza.

Viongozi wa serikali nao kama kawaida yao wakajitokeza na kudai wamepokea KWA MSHTUKO MKUBWA kifo cha Nyaisanga. Salamu za rambirambi zikatolewa kuanzia kwa Mh.Rais Kikwete hadi kwa MaDJs wa Radio Mbao. Wakapiga na nyimbo za kumuenzi mwenzao..

Lahaulah..!! Walikuwa wapi siku zote? Heshima zote hizi kwanini hawakumpa Nyaisanga angali hai, hadi wasubiri kuja kuipa maiti heshima?? Au ndo wanafikisha ujumbe kuwa WANAOKUDHARAU SIKU MOJA WATAKUSALIMIA KWA HESHIMA??

Lakini yote tisa, kumi ni vioja vilivyofanywa na waandishi wenzie. Aliokuwa nao RTD, wengine akaenda nao Radio One, wengine BBC, DW, Sauti ya Amerika etc. Watangazaji maarufu, wenye majina makubwa...wengine huwezi kuwaita majina yao kabla hujatanguliza neno "papaa" kwa sababu wana vitambi vikubwa, cha Idd Amin hakioni ndani..!! Wamekuwa mastar wa mjini..!!

Watangazaji hawa mapedeshee, ambao wengi walidai ni marafiki zake waliingia na mbwembwe Morogoro. Wakabadilisha kila kitu walichokikuta. Wakabadili ratiba ya mazishi na kuweka yao. Wakafuta kamati ya mazishi waliyoikuta Moro na kuunda yao..

Harakaharaka wakaweka na ratiba ya mwili wa Nyaisanga kuagwa Dar, tofauti na kamati ya Morogoro ambayo ilidhani kumuaga Morogoro peke yake ingetosha.

Mapedeshee wakasema lazima mwili wa Nyaisanga uletwe Dar. Watawezaje kuonesha mbwembwe zao mwili ukiagwa Moro?? Magari yao ya Vorgue, Discovery, Lexus hayawezi kwenda Moro. Suti zao kali za Dubai na Hong Kong haziwezi kuchafuka vumbi hadi Moro. Nyaisanga aletwe Dar.!

Waliposhauriwa kuwa mwili wa Nyaisanga ukitolewa Moro, upelekwe Dar kisha upelekwe Musoma kwa kupitia Morogoro utaharibika, hivyo ni bora waage kwa pamoja Moro kisha wapeleke mwili Musoma kwa maziko.. Haraka wakajibu "kama hofu ni mwili kuharibika tutakodi ndege, (Private Jet) itakayopeleka mwili hadi Musoma"

Kwa kauli hiyo Mjane wa marehemu hakuwa na pingamizi. Mapedeshee nao kufika Dar wakatangaza kwa haraka kuwa mwili wa Nyaisanga utaagwa Leaders kisha utasafirishwa kwenda Musoma kwa ndege. Kwa waliomfahamu Nyaisanga na alivyoteseka atleast hii ikawapa faraja kidogo.!

Lakini hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege zaidi ya kutafuta umaarufu tu pale Leaders. Baada ya kuaga, kila mmoja akadisappear na kuachia familia mzigo wa kusafisha maiti kwa gari hadi Musoma. What a shame..!! Kumbe wakati wanajinadi kupeleka mwili kwa ndege akili zao zilikuwa Mabwepande au??.

Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani? Au walikuwa wanatafuta umaarufu? Hii ni dharau..

Nani aliwalazimisha waandishi kuleta maiti Dar na kuja kuitelekeza Leaders?? Kama walishindwa kumheshimu Nyaisanga akiwa hai, kwanini hawakuheshimu hata maiti yake?? Enyi Waaandishi na Watangazaji wa Tanzania, nani aliyewaloga??

Pili, kamati hii ya watangazaji na wandishi iliyoleta msiba Dar waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza na kumweka katika jeneza lingine. Kamati iliyokuwa inaratibu mazishi Morogoro ilimuweka kwenye jeneza alilokuja nalo hadi hospitali ya Muhimbili.

Lakini Kamati ya "Waandishi" wakaenda na jeneza jingine Muhimbili na kumbadilisha Nyaisanga. Mwanakamati mmoja alipohojiwa kuhusu kukataa jeneza la Morogoro alijibu hivi “Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap’ ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi.” (Risasi, 26,October 2013).

Kwa upande wangu this is illogical statement ever made. Ubora uliokuwa unazungumzwa ni nupi? Jeneza lisilo bora lingewezaje kumleta kutoka Morogoro hadi Dar.?? kama ubora walimaanisha nakshi na marembo, ya kazi gani hayo?? Kwanini hizo hela zisingesaidia mjane na watoto walioachwa badala ya kutafuta sifa za kijinga??

Jeneza la gharama ili iweje? Ili tuone kuwa Nyaisanga alikuwa na maisha ya kifahari kumbe sivyo??

Prof.Lipumba aliwahi kusema Watanzania hatuwezi kuendelea kiuchumi kwa sababu tumeendekeza maisha ya bandia. Hatutaki kuishi maisha yetu halisi.. Hatutaki kujikubali.

Mtu anasoma BAED lakini ukimuuliza atakuambia LLB. Hajikubali, atafanikiwaje?? Mtu analipwa Laki 5 kwa mwezi lakini anataka kudrive after two months. Hajikubali.. hataki kukubali kuwa hali yake ni duni na anatakiwa kustrive ili kufanikiwa.

Sasa Nyaisanga amekufa bila msaada wa maana kutoka kwa waandishi wenzie, leo mnamnunulia jeneza la Milioni na ushee, upuuzi..!!

Lakini kama kweli kamati hii ya waandishi walikuwa na uchungu na Julius na hawakutaka awekwe kwenye jeneza cheap, kwanini hawakuungana na kamati ya mazishi ya Morogoro na kuangalia upungufu uliopo na kuurekebisha. Bila shaka wangeweza kuwashauri wenzao wa Morogoro aina ya jeneza la kununua ili wasipoteze hela mara mbilimbili.

Lakini maziko ya Wakristo hufanywa na jeneza moja tu. Jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ndilo hilohilo huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani, tofauti na Waislamu ambao jeneza hurudi msikitini.

Sasa jeneza la Nyaisanga lililokataliwa na Kamati ya Dar litaenda wapi? Mwanakamati mmoja alipoulizwa alijibu kwa kujiamini "Lile tuliliacha Muhimbili ,ndugu watajua cha kufanyia" (Risasi 26, October 2013).

Kwangu mimi hii ni kauli ya dharau. Ndugu watajua cha kufanyia?? What does it mean? Kwamba ndugu walipeleke jeneza nyumbani kujiandaa na msiba mwingine au?

Mi nadhani kamati iliyoundwa Moro ingeachwa ifanye kazi yake bila kuingiliwa kila kitu kingekamilika. Hii kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu. kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma. Mlikuwa wapi Nyaisanga alipokuwa mgonjwa?

Lakini hii si mara ya kwanza mambo haya kutokea kwenye tasnia ya habari nchini. Wapo waandishi wameugua muda mrefu, wameteseka na wengine wamekufa vifo vya mateso, lakini ni nadra kusikia wandishi wenzake wakiripoti habari hizo.

Adam Mwaibabile alifungwa bila hatia, hakuna mwandishi aliyekuwa na habari nae. Hata aliposhinda kesi baada ya kukaa gerezani mwaka mmoja, waandishi wenzie hawakuona ile ni story. Walikuwa busy na story za wanasiasa maana ndio zinamake "headlines"

Hata Mwaibabile alipotoka gerezani na kuandika kitabu chake kuelezea aliyokutana nayo huko jela na namna alivyofungwa kwa uionevu wa RC wa Lindi, hakuna Mwandishi aliyempa suport hata ya kukipa promo kitabu chake.

Hakuna hata gazeti lililodiriki kumpa free space atangaze kitabu chake. Alikuwa akihangaika mwenyewe kama tiara kutafuta market ya kitabu chake.

Hakuna mwandishi aliyemfanyia interview.. Hakuna mwandishi aliyekuwa na muda nae..

Kwani yeye amepigwa risasi na jamaa kutoka Sudan?? kwani yeye amemwagiwa tindikali? Kwani yeye alinyofolewa jicho na kupelekwa S.Africa??

However hata wangedeal nae Mwaibabile hakuwa na 10% ya kuwapa kama waliyozoea kupewa na Wanasiasa kwenye bahasha za khaki..

Wenyewe wanasema si rushwa, bali ni posho tu inaitwa "brown envelop" Huwa wanapewa wakiripoti habari za Vyama vimegoma kukaguliwa fedha za ruzuku, au wakiripoti Mabilioni yaliyofichwa Uswisi..!

Hata hivyo licha ya kuteseka kote huko Mwaibabile akaja kufariki kifo chenye utata na ilidaiwa ameuawa lakini kwa waandishi wenzie ile haikuwa habari kubwa kama ya kukamatwa kwa "Masamaki ya Magufuli"

Waandishi hawakuthamini maisha ya mwenzao kisa Vibua na Pereje za Magufuli ndio ilikuwa "habari ya mjini".

Hadi leo hakuna mwandishi aliyewahi kudevelop story au makala kujaribu kureflect maisha ya Mwaibabile na kifo chake cha utata...

MY TAKE..!!
Waandishi hatuthaminiani.. Hatujaliani.. Hatupendani.. Tumebaki kuchumia matumbo na kutafuta umaarufu wa kijinga mjini. Tupo busy kuripoti habari za wanasiasa na kupiga ramli za kutabiri wagombea urais 2015.

Ifike mahali tujijali na kujipenda. Tujithamini..Tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa.

Tusipojijali sisi hata hao wanasiasa tunaowatetemekea hawawezi kututhamini. wataendelea tu kututumia kama "BIG G" ambayo utamu ukiisha hutupwa, hata aliyekuwa anaitafuna asijue alipoitupa.

MSIBA HUU WA NYAISANGA UWE FUNDISHO KWA WANAHABARI WOTE WA TANZANIA.. (mimi nikiwemo). Tutengeneze image itakayotufanya tukumbukwe hata tutakapoondoka hapa duniani.

Mwanaharakati Che Guevara aliwahi kusema "Im not afraid of death. Because i know when my Heart will beat no more, I wont die. I will continue living in the heart of other people for the Principles, Rules and Beliefs that I lived for..."


Jamal Malinzi achaguliwa kuwa Rais mpya wa TFF!

$
0
0

Rais mpya wa TFF Jamal Emil Malinzi
Habari zilizotufikia Maisha Times zinasema kwamba Jamal Emil Malinzi amefanikiwa kushinda uchaguzi wa TFF kwa nafasi ya urais aliyokuwa anagombea dhidi ya Makamu wa zamani wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani.
Jamal Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.

Serikali yabadilisha Viwango vya Ufaulu Elimu Kidato cha Nne-Sita!

$
0
0
 Katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome


Serikali imebadilisha viwango vya ufaulu wa elimu ya kidato cha nne na sita ambapo daraja la sifuri sasa limefutwa na imeongeza daraja la tano kiwango cha alama ya F ambayo sasa itakuwa alama kati ya 0 hadi 20. Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadililo hayo.

Nchi inayoongozwa na kuendeshwa kwa Matukio aka "Division Five"

$
0
0
Tukiacha matukio mengi yaliyotukia na kupita ni kwamba kwa takribani miezi mitatu vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti habari mbalimbali katika namna ambayo kwa mtu ambaye unafikiri kwa kina na kuona mbali unaweza kugundua jambo fulani kwamba inawezekana yote yanayotukia ni mambo ambayo tayari yamepangwa na hata kutukia kwake ni kwa kufuata series ambayo pale habari fulani inapokomea na kuanza kupotea katika masikio ya wengi ndipo hapo na habari nyingine inapoibuka, Tukianzia na habari ya Rasimu ya mabadiliko ya Katiba sambamba na Muungano wa vyama kadhaa vya kasiasa kushinikiza rais Jakaya Kikwete kutotia saini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na baadae rais Jakaya Kikwete kutoa hotuba ambayo sambamba na mambo mengine pia ilitoa maelekezo kuhusiana na kile vyama pinzani vilichokitaka.

Ilihali habari hiyo ikiwa haijapoa ikatoweka au kutoweshwa ghafla katika masikio ya wengi baada ya kamati ya Bunge ya kusimamia hesabu za mashirika ya umma (PAC) kupitia mwenyekiti wake Zitto Kabwe kuvituhumu baadhi ya vyama vya siasa kwamba kwa takribani miaka minne havijafanyiwa ukaguzi wa hesabu za matumizi ya Ruzuku zinayoipata kutoka Serikalini habari ambayo ilivuma sana kutokana na baadhi ya vyama vingi vya siasa kujibu mapigo ya mwenyekiti huyo wa PAC hususani CHADEMA ambacho kilijitetea vyema na kuthibitisha kwamba tuhuma hizo zilikuwa sio za kweli bali zililenga katika kukichafua kinyume kabisa na sheria zinazohusiana na vyama vya siasa zinavyoelekeza kibaya zaidi ni ikiwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe kuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA habari hiyo iliongelewa sana hata wengine kusema kwamba lengo la Zitto Kabwe lilikilenga chama chake zaidi na wala sio vyama vingine kama wengi walivyokuwa wakidhani, Haikuishia hapo bali ikaibuka habari ya Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia hesabu za mashirika ya Umma (PAC) Zitto kabwe kwenda nchini Uswisi na nchi nyinginezo za bara la ulaya kufuatilia taarifa za Vigogo mbalimbali ambao wanadaiwa kuficha mamilioni yao (Fedha halali na zisizo halali) katika nchi hizo. Habari hiyo ilipokelewa juu kwa juu na kabla hata haijaanza kuvuma muendelezo wa kile wachunguzi wa mambo walichokidai kwamba ni kushindwa kwa mbinu ya kukichafua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia madai ya kutokaguliwa kwa hesabu za matumizi ya ruzuku ya chama hicho kwa miaka minne na muendelezo huo ukaonekana kuunganishwa kwa kitendo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba kukiuka Katiba, Kanuni na Taratibu za chama na kutumia jina bandia mtandaoni kuibua tuhuma nzito akikituhumu chama chake haswa uongozi wa juu wa chama hicho (Katibu na Mwenyekiti) kujihusisha na vitendo vya hila ili kuendelea kuwa viongozi wa chama hicho kinyume na katiba na sera za chama hicho huku akitumia sehemu kubwa ya waraka wake kumsifia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto kabwe karibu katika kila aya ya waraka huo jambo ambalo lilizua migongano na majibishano mitandaoni baina ya wanachama, wapenzi na mashabiki mbalimbali wa CHADEMA hata wale ambao wako kinyume au tofauti na chama hicho hususani CCM ambao daima furaha yao ni kuona CHADEMA inagubikwa na mitafaruku, migongano na makundi ambayo nia kubwa ni kukivuruga chama hicho ambacho kimekuwa tishio hata kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuonekana wazi kwamba kwa namna mienendo ya viongozi wake ilivyo kuna uwezekano kwa chama hicho kuchukua dola katika uchaguzi wa mwaka 2015 kama ambavyo ilithibitishwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete ambaye kutokana na vitendo mbalimbali viovu na vichafu vinavyofanyika ndani ya chama chake alisema "kama rushwa haitakomeshwa ndani ya chama hicho, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015 kitaanguka vibaya na iwapo kitanusurika hakitapita kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amempa jukumu la kushughulikia viongozi wa CCM wanaokula rushwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philipo Mangula.Rais Kikwete, alitoa onyo hilo juzi usiku, alipokuwa akifunga mafunzo maalumu ya siku nne kwa makatibu wa mikoa, makatibu na wenyeviti wa wilaya wa chama hicho nchini.“Kama hatutabadilika katika suala la rushwa mwaka 2015 tutakuwa na wakati mgumu sana na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika Serikali, basi mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani. “Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea shilingi laki mbili za airtime (muda wa mawasiliano), ndugu zangu hatutafika ama wengine watavuka na wengine kukwama,” alisema Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete. Hii ni kauli ya kwanza nzito ya Rais Kikwete ya hivi karibuni ya kukionya chama hicho kuhusu uimara wake wa kuendelea kushika dola.“Viongozi wa chama ndio mmekuwa mawakala wa kusambaza rushwa bila hata aibu. Nawaombeni tubadilike, kama tutaendelea hivi hali yetu itakuwa ngumu sana katika chaguzi mbalimbali, nawaambieni,” alisema Rais Kikwete ambaye alitumia muda wa saa mbili kufunga mafunzo hayo. Aliwaambia kuwa siku hizi watu wana mbadala wa vyama vingine na siyo CCM peke yao.. Aliendelea kusema kuwa tatizo la rushwa kwa viongozi wa chama hicho linazidi kuwa kubwa kila siku, hali ambayo inawapotezea imani wananchi ambao ndio wapiga kura wao.

Ilihali hiyo yote ikiendelea Serikali imebadilisha viwango vya ufaulu wa elimu ya kidato cha nne na sita ambapo daraja la sifuri sasa limefutwa na imeongeza daraja la tano kiwango cha alama ya F ambayo sasa itakuwa alama kati ya 0 hadi 20. Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadililo hayo.Mpaka hapo unaweza kupata picha japo kidogo ni kwa namna gani mambo yanavyoendeshwa au kupelekwa kwa namna ambayo haikupi nafasi wewe kama mwananchi kupata kufahamu mrejesho au muafaka wa kila jambo (Habari) kwa manufaa yako na taifa kwa ujumla kama inavyotakikana na badala yake taarifa au habari nyingi zikionekana kuwa ni za kuibua mambo na kuyaacha hewani badala ya kuyachunguza, kuyaibua, kuyafuatilia na kuyapatia mrejesho na hatimaye suluhisho kwa faida ya wananchi na taifa zima kwa ujumla .

Ushauri wa bure kwa CHADEMA kuelekea 2014-2015!

$
0
0

Kanda ya MASHARIKI Dar es Salaam na Pwani ni miongoni mwa Kanda kumi zilizoundwa ili kukidhi mkakati wa M4C na Chaguzi ndani ya Chama, aidha mfumo huu unatumika kama mwanzo wa utekelezaji wa mapendekezo ya sera ya majimbo ambayo CHADEMA imekuwa ikipendekeza kwenye Ilani yake ya Uchaguzi kipindi cha Kampeni 2010, lengo ikiwa kupunguza Madaraka ya Rais na ukubwa wa Serikali  ili kuharakisha maendeleo kwa kutumia rasilimali za maeneo husika. Kanda zingine ni KUSINI ambayo ni Lindi na Mtwara, KASKAZINI Kilimanjaro, Arusha na Manyara, KANDA YA KATI Morogoro, Dodoma na Singida,  NYANDA ZA  JUU KUSINI Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma, MAGHARIBI Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma, Kanda ya ZIWAMASHARIKI Shinyanga, Simiyu na Mara, ZIWA MAGHARIBI Mwanza, Geita na Kagera na kwa upande wa  ZANZIBAR Pemba na Unguja.
Kamati Kuu katika Kikao cha tarehe 09/11/2012 iliazimia kwamba, mara baada ya Muundo wa Kanda kukamilika na waratibu wa Kanda kuajiliwa, M4C inatakiwa kuongoza zoezi la Uchaguzi  wa ndani ya Chama. Uchaguzi wa Chama unatakiwa kukamilika ndani ya mwaka 2013. Mapendekezo haya yalitolewa mwanzoni mwa mwaka 2011, baada ya kubaini kwamba tunapokwenda kwenye Uchaguzi wa Chama na wakati huo huo kuna Chaguzi za Kiserikali madhalani kuchagua Wenyeviti wa Serikali ya Vijiji/Serikali ya Mtaa  karibu na Uchaguzi Mkuu inaleta mkanganyiko mkubwa ndani ya Chama kama vile kushughulikia rufani mbalimbali  za wagombea ambao kwa namna moja au nyingine hajaridhika na matokeo katika chaguzi ndani ya chama na wakati mwingine kusababisha kukosa ushindi, hivyo msisitizo ukawa Uchaguzi ndani chama unatakiwa ufanyike mapema kabla ya Chaguzi za Kiserikali bila kuathili Utaratibu wa Uchaguzi kama Katiba ya Chadema inavyoelekeza katika Sura ya Sita Ibara ya 6.3.1 (a) – (e) na Muda wa Uongozi Ibara ya 6. 3 . 2 kifungu (a) – (e)
Lakini mpaka naandika makala hii kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu kwa wanachama wengi na baadhi ya viongozi hasa wa Ngazi ya Misingi, Matawi na Kata kuhusu mienendo ya uendeshaji wa shughuli za chama hususani baada ya hizi kanda kuanzishwa, pia kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya chama tangu Uanzishwaji wa hizi Kanda, kumekuwa na Mifumo kandamizi na lazimishi bila kufuata Kanuni, Misingi, Falsafa na Itifaki za CHAMA kwa kuzingatia wajibu na nafasi ya kila Kiongozi katika eneo lake la kazi.
Kuna zoezi la CHADEMA ni MSINGI ambalo limekuwa ni Siri. Na limekuwa siri  kwa viongozi waliopo bila kujua kinachoendelea ni kitu gani ambacho ni Siri katika Ujenzi wa Chama mpaka wengine msishirikishwe. Lakini zoezi limegundulika kuwa ni maandalizi ya kuelekea CHAGUZI za ndani ya CHAMA aidha waendeshaji wa mazoezi haya wanafanya kwa interests zao yaani kujijenga na sio kujenga CHAMA ndio maana hawapiti  kwenye ofisi za Chama wala kuwaona viongozi wa Kata husika. Kwa madai kwamba  wamefundishwa wasiitumie Katiba ya chama kama mwongozo na pia wasipite kwenye Ofisi wala kuuona Uongozi uliopo isipokuwa watumie mbinu kutoka kwenye kitabu cha mafunzo na Programme za Chama kuanzisha Misingi na Brigedi Nyekundu (Kikosi cha Ulinzi) na kamwe wasiwahusishe wadau kama vile Uongozi wa Wilaya/Jimbo au Kata na anayefahamu ni Mbunge pekee na watu wachache waliohudhuria Mafunzo hayo katika Mkoa wa DODOMA,  “anayeona  zoezi hili si shirikishi mlango upo wazi anaweza kujiondoa CHADEMA” je kauli kama hizi za kuogofya ni nzuri kwenye muktadha wa afya ya Demokrasia ? 
Ukitaka kujua njia hata zilizotumika ni haramu na kufanya  zoezi lote kuwa haramu hata namna ya kuwapata watu walioenda kuchukua mafunzo, hakuna waraka wowote kwenda kwenye Majimbo/Wilaya, Kata au Matawi ambayo ndio yenye watu kutoka kwenye Misingi wala hakukua na vigezo vilivyotolewa kwa ajili Ushiriki wa Semina ya Mafunzo. Kwa mfano utaratibu huu uliokiuka Katiba ya Chama umeleta mkanganyiko mkubwa hasa katika Jimbo la Kawe. Aidha haya yote yamefanywa sio kwa bahati mbaya, ni kwa makusudi kwa sababu Jimbo la Kawe ni jimbo ambalo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu dhidi ya ugumu wa kuwandoa viongozi waliokula Fedha za Jimbo ( Ruzuku iliokuwa ikitolewa kila mwezi na Chama ), lakini kuna msemo usemao “usipo stahajabu ya Musa utayaona ya firahuni”,  hao mafisadi  ndio miongoni mwa waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ya CHAMA na ndio  wamekuwa wakufunzi wa CHADEMA ni MSINGI na Kamanda Mkuu wa Red Brigade katika lilelile Jimbo wanalotuhumiwa na hakuna chombo ama Kikao chochote cha Chama kilichowasafisha tangu mwaka jana hadi tarehe 6 mwezi January 2013 wakati Kamati ya Kikosi Kazi ya Jimbo kuundwa. 
Mtindo wanaoutumia ni njia ya kupigiana simu na wakati mwingine kutafuta sehemu iliojificha na endapo watabahatika kumpata mwanachama au mpenzi wa CHADEMA ambao hawajui tuhuma zao katika eneo husika wanamwapisha asitoe taarifa yoyote kwa Mwenyekiti au Katibu wake wa Msingi, Tawi au Kata katika eneo lake kwa gia ya kuwaaminisha kuwa mkakati huo wa programme ya Chadema ni MSINGI ni sawa na Usalama wa Taifa hivyo haipaswi Kiongozi wako kujua wala kuhoji.
 Ki-ukweli na ki-uhalisia zoezi linaloendelea katika Kanda ya Mashariki  Dar es Salaam na Pwani hususani katika JIMBO LA KAWE sijui hali ikoje katika Majimbo ya TEMEKE, UKONGA, ILALA, SEGEREA, KIGAMBONI, UBUNGO na KINONDONI ni zoezi tenganifu na si shirikishi isipokuwa linaleta makundi na migogoro isiyo ya lazima kati ya viongozi waliopo na vikundi vinavyoundwa bila Kamati tendaji za viongozi husika katika Kata au Tawi kwa maana ya Mtaa kushiriki. Jambo hili linaweza likaonekana dogo na kubezwa na Uongozi wa Kitaifa na wakati mwingine hoja zao zinaweza zikapuuzwa  kwa sababu mbalimbali; mfano wa kipuuzi kusema Chama hakipokwenye eneo fulani au kazi haziendi na kufikiri mifumo kandamizi ambayo siyo shirikishi ndio bora katika Ujenzi wa Chama kuelekea 2014 na 2015 Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa na Uchaguzi Mkuu.
Demokrasia ndio Msingi Mkuu wa kutoa haki sio tu ya kuomba Uongozi na kupigiwa kura au fursa ya kupiga kura bali pia kushirikishwa kikamilifu na kutoa mawazo pia kupata taarifa sahihi. Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali kuhusu Ujenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) haioneshi kuwabagua viongozi wa kada mbalimbali katika Chama, lakini hili zoezi la CHADEMA ni Msingi ambayo dhana yake inatokana  na operation za M4C zinaendeshwa kwa minajili ya kuwatenga baadhi yaviongozi ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana wakifanya kazi za Chama bila ya kujipendekeza kwa wabunge au madiwani wao, dhana yao kubwa ikiwa ni kusimamia Falsafa, Kanuni na Misingi ya Chama, aidha wameonekana kuwa mwiba kwa watu wachache wenye maslahi binafsi na kuamua kutumia nafasi au uwezo wao kuwatenga.
Hili jambo limeshaanza kuleta mpasuko na mgogoro mkubwa, na ikiwa viongozi husika wa Kanda ya Mashariki au Makao Makuu wasipofanyia kazi maoni na ushauri wa wadau hasa viongozi linaweza kuwa janga hasa katika Kanda yetu ya Dar es Salaam na Pwani. Nini kifanyike, napendekeza kwamba hatua za haraka zifanyike kwa Wakuu wa Kanda kukutana na Kufanya Vikao vya Majadiliano na wadau ambao watakuwa viongozi wa Jimbo/Wilaya na Viongozi wote wa Kata katika kila Jimbo kwa nyakati tofauti ili kupata njia bora na nyepesi ambayo itawashirikisha viongozi wote bila kuwabagua.
Pili napendekeza pia programu zote katika Ujenzi wa Chama zihakisi mifumo yote ya Kiongozi Kikatiba kwa kufuata na kuzingatia falsafa, kanuni na itifaki za Chama.
Na mwisho ninaonya lugha za kibaguzi kutumika wakati wa kutengeneza team work, mfano kutumia  maneno kwamba, "unajua viongozi wengi ni wakukaimishwa na mamluki" lugha hizo zisitumike au kitendo cha Kiongozi au Mwanachama kusema "mimi tu na fulani ndio tulichaguliwa" iwe kwenye Ngazi ya Wilaya/Jimbo au Kata, haiwezi kuleta dhana ya  ujumla ya kupoka matumizi ya Katiba ya Chama katika shughuli za Ujenzi wa Chama; ikumbukwe kila zoezi la muundo wa Ujenzi wa Chama ikiwemo Chadema ni Msingi ni lazima izingatie mashariti ya: Muundo wa Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unaanza Ngazi ya chini kabisa ambayo ndio Msingi wa CHAMA kwa mujibu wa KATIBA YA CHAMA Ibara ya 7.1.1 ikifuatiwa na Ngazi zingine Tawi Ibara ya 7.2.1 , Kata Ibara ya 7.3.1, Wilaya/ Jimbo la Uchaguzi Ibara ya 7.4.1 , Mkoa Ibara ya 7.5.1 na Ngazi ya juu kabisa ni Ngazi ya Taifa Ibara ya 7.7.1.
Athari na adha ya zoezi hili zimekwisha anza kujitokeza kwenye baadhi ya majimbo mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam inawezekana tukapuuza kama tulivyozoea kujipa matumaini ya kusadikika bila kufanya utafiti au kufika kwa wadau na kuhoji ni nini hasa kinachopingwa katika zoezi hili zuri lisilo na malipo ambalo kila Kiongozi angependa kushiriki kwa uwazi na hatimaye kutengeneza timu nzuri ili kufikia malengo ya Programu ya CHADEMA ni MISINGI kwa wakati.  Tuchukue hatua Mapema
CHADEMA TUMAINI LA WATANZANIA 
Na: Msomaji wetu

Matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2013 ni haya!


Edward Lowassa ana nguvu ya hoja au nguvu ya pesa?!

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Edward Lowassa.

Kwa wale ambao ni wafuatiliaji wazuri wa mambo ya Kisiasa hususani ya nchini Tanzania mtakubaliana na mimi kwamba licha ya changamoto kadhaa alizozipitia katika miaka michache iliyopita akiwa kama Waziri Mkuu wa Tanzania aliyelazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi ni wazi kwamba Lowassa bado ana Nguvu sana, Dakika5 tu alizoongea Bungeni jana zilitosha kubadili uelekeo wa vyombo vya habari nchini... habari ya Division Five ikawekwa pembeni, shinikizo la Spika kujiuzulu ikatupwa kule, Zitto vs Lema ikawekwa kando na vyombo vyote vya habari vikawa vikimzungumzia yeye.

Media karibu zote haswahaswa magazeti yalikabadili upepo wa habari na kuzungumzia kile Lowassa alichokizungumza jana Bungeni kwa muda mfupi tu ambao unakadiriwa kuwa si zaidi ya dakika5, sasa sijui kama Lowassa angeongea kwa masaa mawili ingekuaje! 


Swali ninalotaka kuliuliza ni hili: Edward Lowassa ana nguvu ya hoja au nguvu ya pesa??

Tukiachilia mbali Vituo vya Redio na Television haya ni baadhi tu ya Magazeti ambayo yaliripoti habari katika ukurasa wake wa mbele kuhusiana na Mhe. Edward Lowassa.

Edward Lowassa anatajwa kuwa mmoja ya watu wenye nguvu kubwa sana ya kiushawishi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye kwa harakati na mitazamo yake kuna kila hali kwamba yeye ni moja ya watu kadhaa wanaotajwa kuwa katika nafasi za mbele kabisa za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa octoba mwaka 2015.

• NIPASHE: EDWARD LOWASSA : VIJANA WATATUNG'OA MADARAKANI.

• MWANANCHI: LOWASSA AKOSOA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA.

• TANZANIA DAIMA: LOWASSA AMVAA KIKWETE.

• JAMBO LEO: LOWASSA AMFYATUA KAGAME.

• RAI: LOWASSA AIPA DARASA SERIKALI.

• MAJIRA: LOWASSA ALIPUKA, AWAVAA VIONGOZI.

• HABARILEO: LOWASSA AITAKA SERIKALI KUAINISHA VIPAUMBELE VICHACHE.

• FAHAMU: LOWASSA vs SUMAYE, MEMBE vs SITTA.

• JAMHURI: KINACHONIFANYA NIMPENDE LOWASSA NI HIKI.


Habari Na: Malisa Godlisten

Zitto Kabwe anaudanganya Umma?! Angalia Risiti hii ya Posho!!

$
0
0

Chini ni maneno ya Zitto kabwe kama alivyopost kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo tarehe 2 November 2013!

"Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho. Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao. Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk. Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
Zitto Kabwe

Haya ni maneno ya Zitto Kabwe.. Nanukuu tena "Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao". Mwisho wa kunukuu.

Kama umesoma kwa makini kile alichokiandika Zitto Kabwe (Kwenye ukurasa wake wa facebook) basi linganisha maelezo yake sambamba na tarehe inayoonekana katika Risiti ya malipo hapo juu

Picha Na: Chanzo chetu

Kupata habari zaidi kuhusiana na harakati za Zitto Kabwe katika kupinga posho Bofya hapa....http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/548888-ushahidi-wa-nyaraka-zinazomuhusu-zitto-zuber-kabwe.html

Mitazamo: Mlegezo wa miaka hii sio ule wa miaka ya 1980!

Breaking News: Zitto na Kitila wavuliwa vyeo vyote ndani ya (CHADEMA)!

$
0
0
  
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe
  
Dk. Kitila Mkumbo Mjumbe wa kamati kuu (CHADEMA)

Habari zilizoifikia Blog ya Maisha Times zinaripoti kwamba Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu wote wamevuliwa vyeo vyao vyote walivyonavyo ndani ya chama (CHADEMA) 

Habari kutoka katika chanzo chetu zinaeleza, nanukuu "Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.

Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.

Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama".

Serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68%!

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba. Alisema hayo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. Amsema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.

Mhe Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.

Source: Kumepambazuka, Radio One+JF
Viewing all 209 articles
Browse latest View live