Quantcast
Channel: Maisha Times
Viewing all 209 articles
Browse latest View live

Mandela Dies at 95

$
0
0
May you rest in peace.
Great leader!

Miss Ilala zilipendwa Jacqueline Patrick akamatwa na madawa ya kulevya Macau-China!

$
0
0





Taarifa zilizoifikia maisha Times kutoka katika chanzo chetu zinasema kwamba; Mwanamitindo ambaye pia alikuwa ni Miss Ilala namba 3, mwaka 2005, Jacqueline Patrick amekamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine huko Macau-China. Huu ni mwendelezo wa wimbi la vijana wengi haswa wa Kitanzania ambao wamekuwa wakikamatwa katika nchi mbalimbali kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo haramu na hatimaye kukutwa na madawa hayo ya kulevya.   

Zitto Kabwe: Siko tayari kwa sasa kuwataja Watanzania wenye mabilioni Uswisi!

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe amevunja ukimya na kusema kuwa hayuko tayari kwa sasa kuwataja Watanzania wenye mabilioni huko Uswisi na badala yake ameitaka Serikali ifanye uchunguzi kuhuisiana na suala hilo.

Serikali inajihusisha na Biashara ya Madawa ya Kulevya?!

$
0
0

MIFANO YA KESI ZILIZOHUKUMIWA KULINDA MAKUNDI YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA


Habari hii inatokana na hatua ya Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM) aliyesukuma mashambulizi mazito na akiwatuhumu baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu, watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na Idara ya Mahakama kwa madai ya kushirikiana na wauzaji wa dawa za kulevya, ilizua mshituko mkubwa miongoni mwa jamii.
Katika hoja yake binafsi bungeni mnamo tarehe 04/11/2013 Bulaya alisema baadhi ya watumishi katika ofisi hizo wamekuwa wakishirikiana na watu wanaokamatwa na dawa za kulevya kwa kuwapa siri na mbinu za kuharibu ushahidi ili washinde kesi.
Bulaya alisema: “Kutokana na kupanuka kwa mtandao huu wa kuhujumu, licha ya kushirikiana na washitakiwa, mtandao uliopo katika ofisi hiyo ya DPP umekuwa ukituhumiwa kufanya njama za kushirikiana na baadhi ya watumishi wa mahakama, hasa majaji kuhamisha kesi kupeleka kwa majaji ambao wanadaiwa kuhusika na mtandao huu.”
Wadadisi wa mambo wamedai kuwa hatua ya Bulaya ni ya ujasiri na ameyaweka rehani maisha yake kutokana na uzito wa suala hilo ambalo limekuwa likiitesa serikali kwa muda mrefu.
Wamedai kuwa mbunge huyo ameonyesha ujasiri wa hali ya juu, na kwamba kwa kila namna amewatisha vigogo wanaodaiwa kuhusika na biashara hiyo, hivyo kama asipolindwa na serikali maisha yake huenda yakawa hatarini.
Hofu ya wadadisi wa mambo inatokana na ukweli kwamba, mbunge mwingine kijana wa CCM, Amina Chifupa, aliyekufa miezi michache tu baadaye baada ya kuchachamaa bungeni akiitaka serikali kutaja majina ya wauza ‘unga’ hadharani, huku yeye mwenyewe akiweka bayana kuwa yuko tayari kumtaja hata mumewe, Mohamed Mpakanjia, ikiwa atagundua kuwa anafanya biashara hiyo.
Katika kesi ya Mwinyi Rashid Ismail Mkoko (KLR /IR 4143/2011), mshitakiwa aliomba dhamana Mahakama Kuu wakati kesi ilikuwa bado ipo Mahakama ya Kisutu ndipo wakili wa serikali akamwambia Jaji kuwa anaomba kuifuta.

Alisema Jaji huku akifahamu kuwa kesi hiyo imefika mbele yake kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana tu, na kuwa ilikuwa haijafikishwa Mahakama Kuu kwa utaratibu wa sheria, aliamua kumfutia kesi mshitakiwa na kuamuru kuwa yuko huru. 


Katika kesi Na. 794/2011 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, hakimu aliwafunga kifungo cha nje kwa miezi 15 washitakiwa, Abdulrahman Shaban Sindanema, Said Nassoro Khamis na Abdulrahim Haroub Said waliokiri kosa la kuuza na kusambaza dawa za kulevya aina ya heroin.

Kwa mujibu wa Bulaya adhabu iliyotolewa na hakimu huyu, haipo kwa mujibu wa sheria kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya kuzuia dawa za kulevya, adhabu iliyowekwa kwa wauzaji au wasambazaji wa dawa za kulevya ni kifungo cha maisha na si chini ya miaka ishirini jela kwa kipindi hicho.

Alitoa mfano wa kesi nyingine kuwa ni Na. 274/2005, Jamhuri dhidi ya Yusuph Hashim Nyose, aliyekamatwa na kilo 1.3 za dawa za kulevya aina ya heroin alizokuwa amemeza na kisha kuzitoa kupitia njia ya haja kubwa baada ya kukamatwa na zilikuwa na thamani ya shilingi 12,600,000.

Pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri, ikiwa ni pamoja na mkemia aliyethibitisha kuwa ni dawa za kulevya na mashahidi walioshuhudia mshitakiwa akizitoa kwa njia ya haja kubwa, hakimu alimwachilia huru. 


Kwa kipindi cha miaka mitatu tu (2010-2013), wakati tani 64 za dawa za kulevya zilipita bila kukamatwa…zikiwa mtaani zikiharibu vijana na watoto wetu, katika kipindi hicho hicho kiasi kilichoweza kukamatwa ni tani 1.6 tu!


Takwimu hizo za kutisha zinatoa picha kwamba sehemu kubwa ya shehena za dawa za kulevya hupitishwa bila kugundulika au kukamatwa na vyombo vya dola.”

Mtoa mada alishangaa kwamba ni kwa bahati mbaya, licha ya ukubwa wa tatizo, pamoja na athari zake kwa jamii ya Watanzania, hakuna tafiti zinazoonyesha ukubwa wa tatizo kwa nchi nzima, huku vyombo vya dola vikiwa ndivyo vinara wa kuwatorosha watuhumiwa wanaoendesha biashara hii, ikiwemo ofisi ya DPP na Idara ya Mahakama.

Baada ya mbunge huyo kueleza kwa kina mambo ambayo yanabainisha na kuweka shaka juu ya uadilifu na uaminifu wa watoa haki katika mahakama zetu na ofisi ya DPP na vyombo vya usalama, Sendeka alitaka serikali itoe majibu kuhusu suala hilo la vita dhidi ya dawa za kulevya ambalo si jukumu la Mahakama na vyombo vya usalama pekee bali Tanzania kwa ujumla.

Alibainisha kuwa ili wananchi waweze kujua jinsi waliotoa uamuzi au hukumu ambayo haikuwa kwenye misingi, sheria na mahakama zilivyochukua hatua dhidi ya mahakimu na majaji walio husika.
Mara baada ya Sendeka kumaliza kuomba mwongozo huo, Naibu Spika, Job Ndugai, alitoa fursa kwa Waziri Lukuvi, ambaye alisema serikali inaandaa taarifa inayoeleza jitihada za serikali. “Serikali imejiandaa kutoa kauli kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria na itatoka kabla ya kuondoka hapa bungeni, na itaeleza tulivyojipanga kuunda chombo kipya cha kushughulikia.


Chini ni vyanzo mbalimbali vinavyohusiana na matukio mbalimbali ya Madawa ya Kulevya nchini Tanzania

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Mnigeria-wa-dawa-za-kulevya-hakupita-Tanzania-/-/1597296/1998514/-/1365vslz/-/index.html
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mume-wa-jack-patrick-anaswa
http://www.ippmedia.com/frontend/?l=59073
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1992390/-/x98hm2/-/index.html
http://www.freemedia.co.tz/daima/ester-bulaya-ajilipua/

Wabunge watatu wa CCM wauza "Unga" wajisalimisha!

$
0
0

Baada ya tishio la kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, watu watano wakiwemo wabunge watatu wa CCM wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya wamejisalimisha kwenye kamati ya kidini inayojihusisha na maadili nje na ndani ya makanisa.

Katika mahojiano maalum Mwenyekiti wa Kamati ya maadili na haki za binadamu kwa jamii nje na ndani ya madhehebu ya dini, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga, alitoa taarifa hizo.

Alieleza kuwa wabunge hao (majina yanahifadhiwa) ni wa viti maalum kutoka mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam na Mara. 

Alisema mbali ya wabunge wamo viongozi wa dini na mfanyabiashara maarufu ambaye alikuwa akisafirisha mihadarati mkoani Mbeya.

Mchungaji huyo alisema kujisalimisha huko kunatokana na kamati hiyo mwezi Oktoba mwaka huu kuwataka vinara 61 wakiwemo wabunge hao kujisalimisha kwa ridhaa zao kwa Rais Jakaya Kikwete kama njia ya kutubu makosa yao.

Kinyume na hapo kamati hiyo iliweka wazi uamuzi uliofikiwa kuwa ni kuwapeleka watu hao katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko jijini Hague nchini Uholanzi ili sheria kuchukua mkondo wake.

Mchungaji Mwamalanga alisema kamati ilitoa muda wa miezi miwili ambayo inaisha mwezi huu.

Alisema kutokana na ukaidi huo majina ya watu 56 ya wale ambao hawajajisalimisha ifikapo Januari 15 mwakani yatakabidhiwa rasmi kwenye taasisi za kupambana na dawa za kulevya Umoja wa Mataifa ili wafikishwe ICC.

“Novemba 15, mwaka huu tuliyaingiza majina 61 kwenye mtandao wa taasisi hizo, baada ya hawa watano kuja kwetu, tulipeleka mrejesho kwa taasisi hizi kuwa tumewatoa ingawa nao hawakuenda kwa Rais,” alisema na kuongeza:

“Baada ya kuyaingiza majina haya kwenye taasisi hizi, uchunguzi wa taasisi hizi ulibaini watu hawa ni kweli wanajihusisha na biashara hii, sasa tunachofanya hivi sasa ni kuyakabidhi majina ya wale waliokaidi ili hatua zaidi ziweze kuchuliwa,” alisema.

Alisema kwa sasa kamati ipo katika hatua ya mwisho ya kufanya kazi ya kukusanya majina ya watu waliofariki kwa dawa za kulevya nchini kama ushahidi kwenye kesi hiyo.

Alisema majina hayo wanayakusanya kupitia kwenye hospitali na kwa ndugu wa marehemu waliofariki kutokana na dawa ya kulevya.

Alitaja baadhi ya takwimu walizokusanya za vifo vya baadhi ya watu waliofariki na dawa hizo kwenye mikoa na wilaya kuwa ni Mbeya 38, Kinondoni 67, Dodoma 19, Tanga 41, Lindi saba.

Mchungaji Mwamalanga alisema baadhi ya takwimu hizo ni za mwaka mmoja na nyingine miaka mitatu iliyopita.

Aliongeza kuwa wanaendelea na zoezi la kukusanya takwimu hizo kwenye maeneo mengine.

Kuhusu wale waliojisalimisha kwao ambao gazeti hili inayo majina yao, Mchungaji huyo alisema kamati imewawekea ulinzi wa siri wa kuifuatilia mienendo yao ili kubaini kama wameacha au la kama walivyokiri kwao.

Mchungaji Mwamalanga, alisema moja ya masharti waliyotoa kwa watu hao watano ni kutoa ushirikiano utakaowezesha kukamatwa wale wanaoendelea na kuingiza au kusafirisha nje ya nchi dawa hizo.

Alisema tayari watu hao wameshatoa ushirikiano na kuwezesha kukamatwa watu kadhaa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwenda nchi nyingine duniani.

Alisema watu hao waliwatajia mbinu ambazo hutumika kusafirisha dawa hizo kuwa ni baadhi wamekuwa wakizihifadhi kwenye ‘uume bandia’ na kwenye midoli.

“ Walitueleza kuwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Maziwa Makuu, wafanyabiashara wamebadilisha mbinu za usambazaji wa dawa hizi ambapo njia hizo ndizo hutumika, ukimuona mwanamke kabeba mdoli wengine huwa wamebeba dawa hizi,” alisema.

Pia alisema watu hao waliwaeleza mbinu nyingine ni dawa kusafirishwa kupitia kwa baadhi ya wafadhili wanaoshughulika na mambo ya afya.

Mchungaji Mwamalanga amewaasa vinara hao kuzitumia sikukuu za mwisho wa mwaka huu kujisalimisha wenyewe ili ifikapo mwakani taifa liache kuzungumzia suala hilo.

“Tunawaomba wajisalimishe wenyewe, wanadhani sisi tunafanya mzaa lakini tunawaambia kuwa, watekeleze yale tuliyowataka,” alisema.

Mkutano ambao uliibuka na maamuzi ya kuwafikisha vinara hao ICC ulifanyika siku mbili kuanzia 21 Oktoba mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi wa dini wa madhehebu ya Kiislam na Kikristo 134 kutoka Bara na Visiwani.

Chanzo: Jf
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/576393-wabunge-watatu-wa-ccm-wauza-unga-wajisalimisha.html

Maoni- Zitto abaki au avuliwe uanachama "CHADEMA" Majibu ni haya!

$
0
0

Pichani juu hayo ndiyo Maoni ya Wengi kuhusiana na "KIPIMA BARIDI" Kilichokuwa kikisema: 

Wanaopinga maamuzi ya Kamati kuu CHADEMA na kushauri Zitto Kabwe arudishiwe nyadhifa zake zote na endelee kubaki CHADEMA kama Kiongozi na Mwanachama hai bofya~hit "LIKE" na Wanaokubaliana na maamuzi ya Kamati kuu ya CHADEMA na kwenda mbali na kushauri Zitto Kabwe avuliwe kabisa uanachama piga kura yako kwa kuandika-Comment neno "ONDOA"

HAKUNA UDANGANYIFU WOWOTE UTAKAOTOKEA KWANI WOTE TULIOSHIRIKI KIPIMA BARIDI HIKI TUTASAIDIANA KUKAGUA MATOKEO NA MAJIBU YATATOLEWA KESHO MUDA KAMA HUU. AHSANTENI.

MCHAKATO UNAANZA MARA MOJA NA KUENDELEA. 

Kwa mwendelezo na matokeo zaidi ya wengi waliopiga kura zao katika Kipima Baridi husika bofya Link hapo chini 
https://www.facebook.com/groups/cdmccm/646178402108435/?notif_t=like

Breaking News: Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa amefariki dunia!

$
0
0
 Waziri wa Fedha Mhe, Dr. William Mgimwa

Habari za kuaminika zilizoifikia Maisha Times Blog zinaripoti kwamba waziri wa Fedjha wa Tanzania Mhe. Dr. William Mgimwa amefariki dunia. Habari zaidi zinaripoti kwamba Dr. William Mgimwa amefariki dunia leo katika hospitali ya Mediclinic Kloff nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa 6:20 kwa majira ya Tanzania.




Benki kuu ya Tanzania (BoT) yatoa sarafu maalumu ya Sh. 50,000!

$
0
0

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. 

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.

“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.

Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.

CHADEMA yawavua uanachama Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba!

$
0
0
Dr. Kitila Mkumbo


Samson Mwigamba

Habari kutoka katika chanzo chetu kilichobahatika kupenya na kuingia katika Kikao cha Kamati kuu ya CHADEMA leo tarehe 04.01.2014 saa2:00 usiku zinaripoti kwanba kutokana na kuzijadili kwa kina tuhuma kadhaa zinazowakabili wahusika hatimaye kamati hiyo imefikia hitimisho na kuwavua uanachama Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, hivyo kuanzia sasa Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba sio wanachama wa CHADEMA!

Update ya Press Conference ya leo alasiri tarehe 05.01.2014 kutoka CHADEMA-Makao Makuu

M/Kiti wa Chama Taifa ndio ameingia maeneo haya ya Ofisini akitokea Viwanja vya Karimjee muda wowote kuanzia hivi sasa Mkutano huu na Waandishi wa Habari utaanza rasmi ndugu Wananchi.

Viongozi Wakuu akiwemo Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wameshawasili hapa na sasa Mh. John Mnyika ndio anawakaribisha Waandishi wa Habari na Kutoa salamu za utangulizi

Mnyika anaanza kwa kuomba radhi kwa press kuchelewa anasema ni kwasababu ya uzito wa hoja zenyewe kwasababu Kamati Kuu iliiagiza Sekretarieti kuandaa tamko la leo. Pia Mnyika amewatambulisha Viongozi wa Kanda waliopo mahali. M/Kiti hayupo hapa mbele na badala yake Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa ndie anazungumza na Waandishi wa Habari na tayari ameshaanza kuzungumza.


Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.

Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.


Kuhusu madai ya Mwigamba juu ya kipengele cha Katiba Dr Slaa anaonyesha baraua ya tarehe 13 July 2006 iliyosainiwa na Ndugu Shaibu Akwilombe aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wakati huo kwenda kwa Viongozi wa Mikoa nchi nzima ambayo ilionyesha mabadiliko ya kipengele hicho pamoja na kipengele kilichomruhusu M/Kiti kuteua Manaibu Katibu Wakuu na Katibu Mkuu ambacho kwa makusudi hawakilalamikii kwasababu kilimnufaisha Zitto Kabwe.

Dr. Slaa anamkaribisha Mh. Tundu Lissu ili kuongezea taarifa. Lissu anasema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009 alipokuwa akiwasiliana akina Denis Msack wa Mwananchi. Lissu anasema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare.

Lissu anaongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe ndie amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono wakati Nimrod Mkono alikuwa ni namba sita katika orodha ya Mafisadi iliyotajwa pale Mwembeyanga.


Dr. Slaa anasoma mawasiliano kati ya Zitto na Mtu anayejiita Chadema Mpya. ambapo anasisitiza kuwa Mkakati ulianza kutekelezwa mapema kwa hiyo hoja kuwa Zitto alikuwa hajui Mkakati ni ya Uongo.

Mnyika anamalizia kwa kusema kuwa tuko katika vita dhidi ya maadui wa Chama walioko nje na ndani ya Chama. Hivyo falsafa yetu ya Nguvu ya Umma ndio itakayotusaidia kwa hiyo anatoa wito kwa Wanachama nchi nzima kuitumia falsafa hiyo katika hatua zote ili kushinda vita hii.

Pia anawaomba Wanachama wote kujitokeza kwa wingi mahakamani siku ya kesho katika kusikiliza maamuzi ya Mahakama. 


Mwisho wa Press Conference 

Mbowe: "Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani?"

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Mhe, Freeman Mbowe

"Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali Mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani?"

Chanzo- Gazeti la Raia Tanzania, Jumatatu 6/01/2014

Unaweza kuiongeleaje picha hii??

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe, Freeman Mbowe Kulia na aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA aliyevuliwa nyadhifa zote za uongozi katika chama Zitto Kabwe kushoto!

Tamko la Mhe, Mkono kuhusikana na Tuhuma alizohusishwa nazo!

$
0
0
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM) Nimrodi Mkono

Nimesikitishwa na jinsi Chama kikuu cha upinzani ambavyo kwa siku za hivi karibuni kimeingia katika migogoro ambayo inaathari kubwa kwa ustawi wa demokrasia
hapa nchini.


Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mimi Mh. (Nimrod Mkono) kumpatia Zitto Kabwe (MB) magari mawili (Land Cruiser pamoja na Nissan Patrol). Kwanza napenda ifahamike kwamba sijawahi kumpatia Zitto magari. Isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser; nilitoa msaada wa kuwanusuru kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Zakayo Wangwe (MB) Tarime. Wakiwa wanatishiwa kupigwa (Freeman Mbowe pamoja na Zitto Kabwe) nilijitolea gari langu lenye bendera ya Bunge, liwachukuwe na kuwapeleka Mwanza wakiwa salama, na ilifanyika hivyo. Baada ya kufika Mwanza, Mhe. Zitto aliwasiliana na mimi, kuhusu ununuzi wa gari hilo, nami kupitia kwa wakala wangu Africariers; nilimuuzia Zitto hilo gari.


Kuhusu hilo gari la pili: (Nissan patrol) Mhe. Zitto Kabwe alilikodi, na mpaka sasa anaendelea kulipa vizuri tu; lakini pia ifahamike kwamba hata nyaraka za gari hilo bado ninazo mimi kama mmiliki halali na sijawahi kuhamisha umiliki wake (Transfer of ownership)


KUHUSU KUTOA FEDHA KWA CHADEMA
Nimesikitishwa na ninataka kuweka wazi kwamba, sijawahi kuongea na Tundu Lissu kama inavyodaiwa kwa masuala yoyote binafsi isipokuwa tukiwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.


Ikumbukwe kwamba, nimepita bila kupingwa kwa vipindi vitatu mfululizo (2000, 2005 na 2010). Ni historia ya ainayake; lakini pia uchapakazi wangu kwenye jimbo la Musoma vijijini. Ushindi wangu wa kupita bila kupingwa kwa kiwango kikubwa umekuwa unatokana na bila shaka umahiri wangu kwa kufanya kazi za wananchi kwa kiwango kikubwa.

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon afariki dunia!

$
0
0
Ariel Sharon enzi za Uhai wake

Ariel Sharon ambaye amekuwa kwenye umahututi kwa miaka nane.
Hali yake ilizidi kuzorota katika siku za karibuni na kufanya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi ikiwemo figo zake. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua ugonjwa wa kupooza toka mwaka 2006 wakati akiwa kwenye zama za juu za maisha yake ya kisiasa.
Ariel Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa.
Lakini atasalia kiongozi aliyekuwa na utatanishi mkubwa.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA CHADEMA- FREEMAN MBOWE

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe, Freeman Aikaeli Mbowe

Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza; Tuhuma hizo ni pamoja na; 1.Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo. 2. Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa. 3. Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais. 4. Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni. Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo; 1. Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi. 2. Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala. 3. Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria. 4. Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa. 5. Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani. 6. Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika. Imetolewa leo Dar es Salaam na;

Tumaini Makene Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

Dr. Wilbroad Slaa atajwa na Ujerumani Kama Mwanasiasa Bora Afrika Mashariki

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dr.Wilbroad Slaa

Habari: Katika hali ya Kutia hamasa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dr.Wilbroad Slaa, ameorodheshwa Kwenye Jariba la Uchambuzi wa Masuala ya Kisiasa Nchini Ujerumani Kama Mwanasiasa na Mtu Mwenye Ushawishi Mkubwa zaidi Katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki. Dr.Slaa ambaye amewahi Kuwa Mgombea wa Uongozi wa Juu Kabisa Nchini Tanzania, anaangaliwa zaidi Kwa Jicho la Karibu na Watanzania pia Jumuiya za Kimataifa. Mhariri wa Gazeti la Kila Siku Nchini Ujerumani Bw.Iern Madrne akifanya Mahojiano Katika Jimbo la Bavaria, aliwapa Mtazamo wake Kuhusu Nchi zinazoendelea hususani Nchi za Afrika Mashariki na Kuipongeza Kazi Inayofanywa na Chama Cha Upinzani Nchini Tanzania (Chadema) hata Kufikia hatua ya Kuaminiwa na Watanzania zaidi ya 90%. Dr.Slaa anatarajiwa Kuwa na Ziara ya Kikazi Katika Jimbo hilo la Bavaria Nchini Ujerumani hapo baadae Mwaka huu. 

Tumaini Makene: 0752691569.

Diwani wa CCM na wenzake kizimbani kwa kuchoma basi la Mtei!

$
0
0





Basi la kampuni ya Mtei Express T.742 ACU linavyoonekana baada ya kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali wa kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida, kutokana na kugonga pikipiki aina ya Skygo namba T.368 BXZ na kuua abiria watatu waliokuwa kwenye pikipiki hiyo. 


Diwani wa kata ya Unyambwa mkoani Singida, Shaban Satu-CCM na wenzake 11 watapanda kortini leo wakituhumiwa kuchoma moto basi la Mtei na kusababisha hasara ya Shilingi za kitanzania Milioni 70.

Siku ya Tukio
Basi hilo lilikuwa likitoka Singida  kuelekea Arusha ambapo watatu wa familia moja walifariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongwa na kuburutwa na basi la kampuni ya Mtei Express ya mjini Singida.

Watu hao ni Tamili Shaban na Kassimu wamefariki dunia papo hapo kwenye eneo la tukio ambalo ni kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Manispaa ya Singida. Hamza amefariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Singida. Miili ya watu hao ilihifadhiwa katika chumba cha mochwari katika hospitali ya mkoa.

Baba mzazi wa watoto hao, Shaban Bunku ambaye imedaiwa ni mlinzi wa kampuni ya TTCL mjini hapa,alilazwa katika hospitali ya mkoa na hali yake ni mbaya. Inadaiwa alivunjika mguu wa kulia na damu zilikuwa zikimtoka kichwani.

“Dereva wa basi hilo alilazimika kusimamisha basi hilo kutokana na kuburuta pikipiki hiyo. Baada ya kusimamisha basi hilo wananchi wa eneo hilo walipigiana simu na ghafla walijaa na kuanza kuvunja vunja vyoo na kisha kilichoma moto”,amesema Kamwela.


Picha ya Wiki!

Unaweza kuizungumziaje Picha hii??

Msanii wa Tamthilia ya Isidingo- Lesego Motsepe "Letti Matabane" Amefariki Dunia!

$
0
0
Marehemu Lesego Motsepe "Letti Matabane"

Msanii wa tamthilia ya Isidingo the Need Lesego Motsepe "Letti Matabane" amefariki jana nyumbani kwake Randburg nchini South Africa. Taarifa kutoka kwa msemaji wa familia Moemise Motsepe ambaye ni kaka wa Marehemu amesema kwamba alikwenda nyumbani kwa dada yake yapata muda wa saa5 asubuhi na kuukuta mwili wa dada yake ambaye alikuwa ameshafariki masaa kadhaa yaliyopita (Kulingana na vipimo vya Dakrari).

Miaka kadhaa iliyopita Lesego Motsepe "Letti Matabane" aliwahi kujitangaza kwamba ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na amekuwa akiishi kwa matumaini kwa zaidi ya miaka 13 na katika kipindi chote hicho hakuwahi kutumia vidonge vya kurefusha maisha (ARV's).

Wengi wanamzungumzia Lesego Motsepe "Letti Matabane" kwamba ni msichana aliyekuwa mcheshi mchangamfu na asiye na majingambo.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Lesego Motsepe "Letti Matabane"

Source: 


Mbunge wa jimbo la Chalinze afariki dunia!

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Marehemu Ramadhani Bwamdogo

Habari zaidi zinasema kwamba Marehemu Ramadhani Bwamdogo amefariki leo tarehe 22/01/2014 katika Hospital ya Moi alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema Peponi Amina.



Viewing all 209 articles
Browse latest View live